Home » » Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid-El-Fitri

Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid-El-Fitri

Written By CCMdijitali on Tuesday, July 5, 2016 | July 05, 2016

Kwa ufupi

Akizungumza leo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir alisema mbali na baraza hilo litakalofanyika saa 10.00 alasiri, Swala ya Idd kitaifa itaswaliwa saa 1.30 asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.


By Suzan Mwillo, Mwananchi smwillo@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid-El-Fitri litakalofanyika kesho katika viwanja vya Karimjee jijini hapa.
Akizungumza leo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir alisema mbali na baraza hilo litakalofanyika saa 10.00 alasiri, Swala ya Idd kitaifa itaswaliwa saa 1.30 asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
“Waumini wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya swala. Walioko maeneo mengine wajitokeze kwa wingi misikitini,” alisema Sheikh Zubeir.
Sheikh Zubeir alisema viongozi mbalimbali akiwamo, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, wanatarajiwa kuhudhuria kwenye ibada hiyo.
Mufti alitoa wito kwa waumini wa dini hiyo kusherehekea sikukuu ya Idd kwa amani huku akiwaasa waumini wa dini hiyo kuendelea na kutenda matendo mazuri waliyojifunza wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
“Katika miezi ijayo tuendelee na matendo mema,” alisema.

Kuandama kwa mwezi

Akizungumzia kuandama kwa mwezi, Mufti Zubeir alisema waumini ya dini ya Kiislamu kesho wataungana na wenzao kote duniani kusherehekea Sikukuu ya Idd baada ya mwezi kuandama jana.
Alisema kwa Dar es Salaam, mwezi ulionekana jana Mbagala na baadhi ya maeneo kadhaa ya mikoani.
Waumini wa Kiislamu walikuwa katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni kutekeleza moja ya Nguzo Tano za dini hiyo.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link