Home » » Tanzania ndani ya nne bora za China

Tanzania ndani ya nne bora za China

Written By CCMdijitali on Tuesday, July 5, 2016 | July 05, 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa

Kwa ufupi

Hayo yamebainika kwenye kongamano la wachumi na wadau wa biashara kati ya China na Tanzania, Kenya na Afrika Kusini ambalo lilijadili fursa na changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.

By Julius Mathias, Mwananchi jmathias@mwananchi.co.tz



Dar es Salaam. Tanzania ni kati ya nchi nne ambazo Serikali ya China imeahidi kufanya ‘kufuru’ ya uwekezaji wa viwanda.

Hayo yamebainika  kwenye kongamano la wachumi na wadau wa biashara kati ya China na Tanzania, Kenya na Afrika Kusini ambalo lilijadili fursa na changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ambaye alikuwa anafungua kongamano hilo, amesema uamuzi wa kuiteua Tanzania ulifanywa kwenye mkutano uliofanyika mapema mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Amesema katika mkutano huo ambao Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, China iliamua kushirikiana na nchi za Afrika Kusini, Kenya na Tanzania kujenga uchumi wa viwanda.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link