Home » » Waziri Ummy Mwalimu afanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Waziri Ummy Mwalimu afanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Written By CCMdijitali on Tuesday, July 19, 2016 | July 19, 2016

 
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora akiongea na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipoenda kumuaga rasmi ofisini kwake Dkt.Chatora amemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Tanzania na hivyo kuhamishiwa nchini Afrika ya Kusini

Waziri Ummy Mwalimu akifanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora Dkt.Chatora amesisitiza wizara kujenga uwezo wa ndani katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kwa kushirikiana na wizara ya maji, mazingira pamoja na elimu.

Vile vile alishauri Serikali kuongeza nguvu katika huduma ya mama wajawazito pamoja na kuwekeza katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo hivi sasa yanaongezeka kwa kasi na kuathiri jamii amemshukuru kwa ushirikiano wake katika sekta ya afya tangu awepo nchini na ameahidi kuendelea kutekeleza yale yote aliyoishauri wizara

(Picha na Wizara ya Afya)
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link