Waamuzi wa Mchezo wa leo kati ya Yanga ya Tanzania na Medeama ya nchini Ghana, wakiziongoza timu kuingia uwanjani tayari kwa kuanza kwa mchezo huo wa Kombe la Shirikisho, uliopigwa kwenye Dimba la Taifa jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana Bao 1-1. ambapo Goli la Yanga liliwekwa kimyani na Mshambuliaji Donald Ngoma dakika ya pili tu ya Mchezo kipindi cha kwanza huku Medeama wakisawazisha dakika 17 baadae kupitia mwa Mshambuliaji wake Benard Danso.
Kikosi cha Medeama.
Kikosi cha Yanga.
Wachezaji wa timu ya Yanga, wakishangilia ushindi wao pamoja na Washabiki wao, baada ya Mshambuliaji wake Donald Ngoma kuipatia timu yake goli la kuongoza ikiwa ni dakika ya pili tu Mchezo dhidi ya Medeama ikiwa ni Mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Washabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao.
Kipa wa Yanga, Dennis Munishi "Dida" akiiunyaka mpira kwa umaridadi kabisa.
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Medeama, Samuel Adade.
Mwamuzi wa Mchezo huo, Ibrahim Nour El Din akimzawadia kadi ya njano, beki wa Timu ya Medeama.
Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akijiandaa kuachia shuti kuelekea langoni mwa Timu ya Medeama, wakati wa Mtanange wa Kombe la Shirikisho, uliopigwa Uwanja wa Taifa leo. timu hizo zimetoka sare ya kufungana 1-1.