Home » » Balozi Seif Ali Iddi azungumza na Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon

Balozi Seif Ali Iddi azungumza na Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon

Written By CCMdijitali on Friday, August 12, 2016 | August 12, 2016

 Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar alipofika kujitambulisha rasmi kuanza kazi zake za Kidiplomasia hapa Zanzibar.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akizungumza na Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon aliyepo kati kati alipofika kujitambulisha rasmi.

Wa kwanza kutoka kushoto ni msaidizi wa Balozi  Xie Xiaolon anayeshughulikia Utawala Bwana Wang Xingjun.



Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon akibadilishana mawazo na Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Picha  na – OMPR – ZNZ.


                                       Press Release:-



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba  Zanzibar inaendelea kufaidika kiuchumi na Maendeleo kutokana na kuungwa mkono kimisaada kutoka kwa mshirika wake mkubwa wa maendeleo Jamuhuri ya Watu wa China.

Alisema China imekuwa mshirika wa karibu na Zanzibar hasa katika sekta ya Kilimo na Viwanda ulioanza mara baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 ambao umewezesha kufungua  milango ya ajira kwa Vijana waliowengi Visiwani Zanzibar.

Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akizungumza na Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo  Zanzibar Bwana Xie Xiaolon aliyefika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambalisha rasmi kushika wadhifa wa mtangulizi wake Bwana  Xie Yunliang aliyemaliza muda wake.

Alisema ujenzi wa utanuzi wa eneo la maegesho ya Ndege, Bandari ya Mpiga Duri Maruhubi, Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee Mkoani Pemba pamoja na uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Kisasa ya mtandao wa Mawasiliano { E. Government }ni miongoni mwa Miradi Minne mikubwa inayofadhiliwa na China kupitia Benki ya Kimataifa ya Exim.

Balozi Seif  kupitia Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China na Benki hiyo kwa kuendelea kuiunga Mkono Zanzibar katika miradi  hiyo ya Maendeleo, Kiuchumi na Ustawi wa Jamii.

Alisema hatua hiyo itazidi kuimarisha uhusiano wa pande hizo mbili uliodumu kwa takriban miaka 52 sasa ambao unazidi kukuwa kadri maisha ya Wananchi wa sehemu hizo yanavyoendelea kuingiliana Kibiashara na Kiutamaduni.

Aidha Balozi Seif alifahamisha kwamba mabadiliko ya haraka ya kiuchumi yanayoendelea kufanywa na Taifa hilo kubwa la Bara la Asia yataendelea kutoa nafasi kubwa zaidi kwa  Nchi changa zinazoendelea hasa zile za Bara la Afrika kuiga mfano huo.

Mapema akijitambulisha rasmi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha miradi iliyoanzishwa Zanzibar na kupata msukumo wa kiuwezeshaji kutoka Nchini Mwake inakamilika kwa wakati.

Balozi Xie alielezea faraja yake kutokana na Uongozi wa  Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya ZTE yenye Makao Makuu yake  Nchini China uliofadhili mradi wa uwekaji  wa Taa za bara barani zinazotumia mwanga wa Jua kuanzisha mpango maalum wa kuzifanyia matengenezo taa hizo.

Alisema zipo baadhi ya taa tayari zimeanza kuleta hitilafu zinazopelekea kushindwa kufanya kazi zake kama kawaida za kutoa mwanga kwenye bara bara kutokana na uchakavu wa betri zake.

Ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wananchi wake kwa kuendelea na harakati zao za kimaisha katika misingi ya amani na utulivu mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Balozi Xie alieleza kwamba hatua hiyo itatoa fursa kwa Viongozi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla pamoja na Jamuhuri ya Watu wa China kuendelea kishirikiana kwa maslahi ya pande hizo mbili.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
12/8/2016.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link