Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubiga akizungumza na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya siku ya jeshi hilo nchini itakayoadhimishwa Septemba Mosi, mwaka huu. Kulia ni Ofisa Habari wa jeshi hilo, Said Ndimbo. Picha na Said Khamis
Kwa ufupi
Siku hiyo, JWTZ watafanya usafi kwenye maeneo mbalimbali na kutofanya maandamano kwa kuwa Serikali imeyazuia.
Dar es Salaam. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litaadhimisha miaka 52 ya kuanzishwa kwake Septemba Mosi.
Siku hiyo, JWTZ watafanya usafi kwenye maeneo mbalimbali na kutofanya maandamano kwa kuwa Serikali imeyazuia.
Jeshi hilo liliundwa upya Septemba 1964 baada ya kuvunja jeshi lililorithiwa kutoka ukoloni la Tanganyika Rifles ambalo liliasi Januari 20, 1964.
“Sisi wanajeshi tukipanga shughuli zinakwenda jinsi zilivyopangwa, ratiba yetu ni kusherehekea, tunajua Serikali imeshakataza maandamano,” amesema msemaji wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga kwenye makao makuu ya jeshi hilo jijini hapa.