KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi Mlonge/mlongo/ mronge, mrongo/mkimbo au mzunze (kwa Kiingereza unaitwa Moringa Oleifera ) unaweza kuwa unaongoza.
Kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu ingawa kwa bahati mbaya sana huenda wengi hatuujui ima tunaujua na kuupuzia. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, mti wa Mlonge unatibu karibu magonjwa 300 ya aina mbalimbali, yakiwemo yale magonjwa sugu.
Profesa Mmoja wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) amenukuliwa akisema “imethibitishwa na kufanyiwa utafiti kupitia Idara ya Sayansi na Chakula iliyopo SUA na kugundua kuwa mti wa mlonge ni mti muhimu sana katika jamii na una faida nyingi.”....
Mlonge unaweza kutibu Pumu, Kikohozi na Kifua Kikuu. Aidha, magonjwa mengine kama Kisukari, Shinikizo la damu, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya kwenye njia ya mkojo (UTI) kuongeza kinga ya mwili (CD4) na kuongeza nguvu za kiume.
Mbegu za Mlonge hutibu maradhi pia kama Malaria, Saratani ya tumbo, hupunguza sonona stress, huleta hamu ya kunywa maji, jambo amabalo ni adimu kwa watu wengi
Faida nyingine itokanayo na unga wa majani ya mti wa mlonge ni kusafishia maji ambayo ni machafu na kuweza kuwa safi na salama na kuwa tayari kwa matumizi yoyote ya nyumbani kama vile kupikia na kunywa, hii inaweza kuwa ni mbadala ya madawa mengine yanayoweza kutibu maji kama vile watergard na mengineyo.
Majani ya Mlonge yamepachikwa jina la chakula chenye viwango kwasababu wanasayansi waligundua yana kiasi cha madini ya Kalisium yanayoweza kupatiakana katika glasi nne za maziwa, kiasi cha vitamini c inayopatikana kwenye machungwa saba, Potasium ya kwenye ndizi mbivu tatu. Pia unapata kiasi cha madini ya chuma mara nne zaidi.
Majani ya Mlonge yana Vitamin A nyingi kuliko karoti, vitamin C nyingi kuliko machungwa na madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu, halikadhalika ubora wa protini yake ni bora kushinda maziwa na mayai.
Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya chuma (Iron), kasiamu (Calcium) na vitamin nyingi za aina mbalimbali, majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’ kwa watoto wadogo na vijana ili kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.
Majani mabichi ya Moringa ni mazuri kwa kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia.
-Juisi ya majani ya Moringa hutumika kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi ikichanganywa na asali inatibu kuharisha.
Pia juisi ina uwezo wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye kisukari.
-Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.
-Waweza kutumia majani kama unavyotumia mchaichai na hapo unatibu MALARIA bila kujua.......Majani ya Mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi (zingatia usikaushe kwenye JUA)
Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.
Licha ya kuwa dawa nzuri sana ya kusafisha tumbo (Jaribu kutafuna mbegu zake tatu baada ya kumenya huku ukinywa maji mengi sana na kuhakikisha upo jirani na choo) Mbegu za mti wa Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.
Pia mbegu hutuminka katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa baada ya kuchemsha.
Magome
Magome ya mti wa Moringa hupondwa na kuwa rojorojo kisha hutumika kutibu majipu pia hupakwa ili kupunguza maumivu yatokanayo na kung'atwa na wadudu kama nyoka na nge. mmea huu pia ni MBOLEA
...........HIZI NI BAADHI TU LAKINI WAWEZA JISOMEA ZAIDI KUPITIA VYANZO MBALIMBALI ..............
Ndugu tuna tabibu mbalimbali, za asili na zisizo na madhara kama ya vidonge vya makemikali na bado tunapuuza.
Nimekuwa nikiusikia huu mmea leo umepata undani matumizi yake.
ni zao zao rahisi kupanda unapanda umbali wa mita 3 unapanda punje mbili kila shimo ikiota vizuri unang'oa moja baada ya miezi 9 inaanzakuzaa unavuna x2 kwa mwaka mlonge unazaa sana ila kung'oa mlonge sio kazi rahisi una kiazi ambacho hakifi
imeandikwa na Geofrey Chambua kutoka vyanzo mbalimbali