Home » » MAMA SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA PILI NA MAONESHO YA KITENGO CHA WAHANDISI WANAWAKE CHA TAASISI YA WAANDISI TANZANIA

MAMA SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA PILI NA MAONESHO YA KITENGO CHA WAHANDISI WANAWAKE CHA TAASISI YA WAANDISI TANZANIA

Written By CCMdijitali on Friday, August 12, 2016 | August 12, 2016


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan aonyesha zawadi ya Saa aliopewa na Wahandishi Wanawake (TAWESE) kwenye Kongamano la Pili la Maonesho ya Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Mhandisi Mshauri Bi. Warda Ester Mash'mark alipotembelea banda lake wakati wa Kongamano la Pili la Maonesho ya Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Anifa chingumbe wa TTCL namna ambavyo mtandao wa 4G LTE unavyofanyakazi alipotembelea banda la TTCL kwenye Kongamano la Pili la Maonesho ya Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
 

Sehemu ya Waandishi waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais.

 
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wahandisi wanawake nchini kufanya kampeni maalum ya kushawishi watoto wa kike kujenga ari ya kusoma masomo ya sayansi na hisabati kama hatua ya kuongeza maradufu wahandisi wanawake nchini.

Makamu Rais ametoa kauli hiyo 12-Aug-16 wakati anafungua kongamano la maonyesho ya kitengo cha wahandisi wanawake cha Taasisi ya Wahandisi Tanzania katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Amesisitiza kuwa kampeni hiyo itasaidia kuelimisha wasichana,kuwaunganisha na kuwaendeleza watoto wa kike ili waweze kujitambua na kuithamini nafasi yao katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia fani za sayansi na teknolojia.

Makamu wa Rais amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa wahandisi katika maendeleo ya nchi hususani katika sekta za nishati,madini,barabara,maji,uvuvi na kilimo imeendelea kuweka mipango madhubuti ya kuinua na kuimarisha fani ya uhandisi hapa nchini.


Copyright: Michuzi Blog
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link