Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo. |
Kwa ufupi
- Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi Kamambe wa Kuimarisha Usambazaji Umeme Vijijini (TREEP) awamu ya pili katika Kijiji cha Kwedizinga, Kata ya Kabuku wilayani Handeni kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (WB), Muhongo amesema Serikali inataka kila mwananchi atumie nishati hiyo nyumbani.
Handeni. Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo amewataka wakulima wa mboga na matunda kutumia fursa ya umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) kufungua miradi na viwanda vidogo vya usindikaji vyakula.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi Kamambe wa Kuimarisha Usambazaji Umeme Vijijini (TREEP) awamu ya pili katika Kijiji cha Kwedizinga, Kata ya Kabuku wilayani Handeni kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (WB), Muhongo amesema Serikali inataka kila mwananchi atumie nishati hiyo nyumbani.
“Mahindi na mpunga mtakoboa hapa hapa hamtaenda tena mjini, wanunuzi watakuja kwenu na mtawauzia kwa bei mnayotaka tofauti na sasa kwa sababu hamna umeme,” amesema.