Na Mwandishi Wetu - Arusha
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha
wamevunja kikao cha Baraza la Madiwani kilichokua kinafanyika leo asubuhi 29/08/2016
kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa maslahi ya chama chao (CHADEMA) na
kutupilia mbali shida na kero za wananchi waliowachagua.
Walinukuliwa mara baada ya kuvunja kikao hicho,wakitoa
sababu ambazo,zilionekana kutokuwa na
mashiko kwa maslahi ya Wananchi au wapiga kura wao.
Baadhi ya sababu walizozitoa ni :-
- Kuna madiwani 8 wanaotafutwa na Jeshi la Polisi,hivyo kuhofia kukamatwa ,endapo wangefika kwenye kikao hicho.
- Walihitaji kwenda kuwawekea dhamana baadhi ya Viongozi wa Chama chao
- Kuhudhuria kesi inayomkabili Godbless Lema inayotarajiwa kusikilizwa leo machana
Mahakamani
Hivi ninajiuliza ,sababu hizi zina umuhimu wowote wa
mustakabali wa Wananchi wa Jiji la Arusha ? Jibu hapana ! Na sababu ziko wazi
tu.
i.
Je katika Jiji la Arusha,hakuna watu
wenye sifa za kuweza kuwadhamini Viongozi hao ?
ii.
Je Jeshi la Polisi limeshindwa
kuwafikia mahali walipo, ikiwa Godbless Lema
(Mbunge ) amekamatwa, sembuse wao ?
iii.
Hivi kweli kwa akili za kawaida,
iwapo kikao kilikuwa ni asubuhi na Godbless Lema anapelekwa Mahakamani Mchana,
je walishindwa kuendelea na kikao hicho kwa masaa waliyokuwa nayo?
iv.
Hivi kweli dhamana iliyohitajiwa ni
ya Madiwani wote 33 wanaotokana na Chama cha Demokrasia (Chadema) ?
Ili kikao kiendelee ,kilihitaji kiwe
na angalau Madiwani wasiopungua 17,lakini pia walishindwa kuona umuhimu wa
Baraza hilo,kwani mambo ya msingi na maendeleo yangeweza kujadiliwa na wengine
wangeweza kwenda kushughulika na masuala ya kesi na dhamana za viongozi wao.
v.
Hivi tujiulize Kikao cha
robo ya tatu ambacho kinategemewa kutoa maazimio muhimu na kupitisha miradi
mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya Utekelezaji ili kuleta maendeleo kwa
wananchi kinavunjika kwa sababu ya kuhudhuria kesi ya mtu mmoja na
madai eti wanatafutwa na Polisi ?
vi.
Zaidi ya yote
Halmashauri imetumia gharama kubwa na muda mwingi kwa watumishi wake kuandaa
kikao hicho,pamoja na gharama za kupeleka Makabrasha kwa madiwani wote ambapo
Magari yake yametumika kusambaza Makabrasha kwenye Kata zote na kutoa matangazo
kwa ajili ya Kikao hicho, lakini yote hayo hawakuyathamini na kuamua kuvunja kikao hicho kwa sababu zao binafsi.
MTAZAMO
WA KIZALENDO
Ifike mahali busara na Uzalendo upewe kipaumbele katika masuala
ya msingi na ya lazima yanayohusu Maendeleo na mustakabali wa Jiji letu la Arusha.
Ni wazi Madiwani wa Arusha hawakuchaguliwa na kikundi cha watu
wachache wanaonekana kuwa bora au muhimu zaidi ya Wananchi waliowachagua.
Haingii akilini kesi ya mtu mmoja ambaye ni ya kujitafutia
mwenyewe iingizie hasara serikali na kusababisa shughuli na mipango ya
maendeleo ya Jiji la Arusha kusimama.
Itakuwa haina maana Halmashauri ya Jiji la Arusha kufanya
kazi kwa maslahi ya Chama cha siasa(CHADEMA) badala ya maslahi ya wananchi na
wakazi wa Jiji la Arusha.
Ninukuu kauli ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli,ambayo amekuwa akihimiza na kuirudiarudia kila alipopata fursa ya kuongea na Wananchi kuwa “MAENDELEO HAYANA CHAMA”
Kila mwanachama wa Chama chochote cha Siasa na wale
wasiokuwa na Chama,wanahitaji Maendeleo. Kwa sababu hiyo,kila mmoja napaswa
kufanya kazi kwa kuweka maslahi ya Wananchi wote mbele.
Kwa hicho walichokifanya Madiwani wa Chadema chini Mstahiki
Meya Lazaro , hakikubaliki na kinasthili kuchukuliwa hatua za kisheria na
kikanuni na kukemewa kwa nguvu zote na Wanachi wote wapenda wa Jiji la Arusha.
ARUSHA BILA UBINAFSI INAWEZEKANA.