ALIYOYASEMA EDWARD MORINGE SOKOINE
Written By CCMdijitali on Sunday, September 4, 2016 | September 04, 2016
Labels:
KITAIFA
#Kaziiendelee
Kaulimbiu | Desemba 09,2016“Tuunge mkono jitihada za kupinga rushwa na ufisadi na tuimarishe uchumi wa viwanda kwa maendeleo yetu.”
Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara
"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta:
"Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa
"Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe
"Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe.
"Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi.
"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda
Kuzaliwa: 01/08/1938
Kitongoji cha Kilasho, Kijiji cha Emairete, Monduli Juu.
Wazazi: Baba Sokoine Ole Severe
Mama Napelel Sinyati Noomoyaki-Sokoine
Elimu ya Msingi: 1949-1953 Monduli Primary School
1953-1956 Monduli Middle School
Elimu ya Sekondari: 1957-1958 Umbwe Secondary School
Elimu ya Juu:
1962-1963 Mafunzo ya Maofisa Watendaji, Mzumbe
1963-1964 Akiwa Executive Officer alihudhuria mafunzo ya watumishi wa serikali za mitaa nchini Ujerumani
1981-1982 Alijiunga na Chuo Kikuu cha Belgrade, kusomea Uchumi wa Kijamaa alifuzu na kutunukiwa Diploma ya Juu.
1983 Chuo Kiku cha Dar es Salaam (UDSM) kiliyatathmini masomo hayo aliyoyafanya na kuyatambua kuwa ni sawa na shahada ya Bachelor of Arts (BA)
1983-1984 Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuchukua masomo ya shahada ya juu ya sayansi ya siasa. Alifariki akiwa amebakiza sura moja kumaliza Thesis yake.
Siasa
Januari 1, 1961 Alijiunga na Chama cha TANU
Februari 5, 1977 Alikuwa mwanachama mwanzilishi wa CCM ilipoanzishwa
1977-1984 Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM
1982 Katibu wa Tume ya Ulinzi na Usalama
Uongozi
1961-1962 Alijiunga na Serikali za Mitaa kama msaidizi wa Katibu wa Halmashauri ya Shirikisho la Masai (Masai Federal Council), baada ya muda mfupi alipandishwa cheo kuwa Katibu wa Halmashauri ya Shirikisho la Masai.
1963 Baada ya masomo Mzumbe Training Centre, aliteuliwa kuwa Ofisa Mtendaji Daraja la nne.
1965-1970 Mbunge wa Jimbo la Maasai (lililojumuisha majimbo ya sasa ya Ngorongoro, Longido, Monduli, Simanjiro na Kiteto).
1967 Aliteuliwa kuwa Waziri Mdogo (Naibu Waziri) wa Mawasiliano, Uchukuzi na Kazi.
Novemba 1970 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu.
1970-1980 Mbunge wa Jimbo la Monduli (lililojumuisha majimbo ya sasa Monduli, Longido na Ngorongoro).
Februari 1972 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
13/02/1977 -07/11/1980 Aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Novemba 1980 Alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu, kwa sababu za kiafya.
1980-1984 Mbunge wa Jimbo la Monduli (Monduli na Longido ya sasa)
Februari 24, 1983 Aliteuliwa kwa mara ya pili kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nafasi aliyoishika hadi kifo chake Aprili 12, 1984
Marehemu Edward Moringe Sokoine alifariki dunia akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Katibu wa Baraza la Ulinzi na Usalama, Mjumbe wa Kamti Kuu na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.