Home » » Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli waweka mashada ya maua katika kaburi la Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi

Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli waweka mashada ya maua katika kaburi la Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi

Written By CCMdijitali on Saturday, September 3, 2016 | September 03, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Septemba, 2016 ameendelea na ziara yake Visiwani Zanzibar ambapo majira ya Asubuhi amezuru Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume lililopo kando ya Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) eneo la Kisiwandui Zanzibar.


Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika Kaburi hilo na baadaye wameshiriki Dua ya kumuombea Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume na kuombea amani.

Viongozi mbalimbali wa Dini na Siasa akiwemo Rais Mstaafu wa Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume ikiongozwa na Mjane wa Marehemu Mama Fatma Karume wamehudhuria.

Baada ya kuzuru kaburi la Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume, Rais Magufuli amezuru kaburi la Rais wa Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi lililopo nyumbani kwake Migombani Zanzibar.

Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika kaburi la Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi na pia wametoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu.

Wakizungumza katika Dua ya kuwaombea Marehemu wote wawili Viongozi wa Dini kutoka madhehebu ya Kiislamu na Kikristo wameomba kuwepo kwa amani na upendo kwa watanzania wote kama ambavyo waasisi wa Taifa walipigania.

Baadaye leo Rais Magufuli atazungumza na Wananchi wa Zanzibar katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Demokrasia wa Kibandamaiti Mjini Zanzibar.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Unguja

03 Septemba, 2016.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akitoa heshima zake baada ya akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
 Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
 Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  na viongozi wengine wakiomba dua bada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  na viongozi wengine wakiomba dua bada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli, akiwa na Mama Fatma Karume baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Septemba 3, 2016.
 



Picha na Ikulu

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link