Home » » Kigwangalla afanya ziara Hospitali za Wilaya ya Mlele na Mpanda Mkoani Katavi

Kigwangalla afanya ziara Hospitali za Wilaya ya Mlele na Mpanda Mkoani Katavi

Written By CCMdijitali on Thursday, September 29, 2016 | September 29, 2016

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, 
Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mlele na 
kutembelea Hospitali ya Mlele ya Wilaya hiyo pamoja na Hospitali ya Mpanda iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi huku akitoa maagizo mbalimbali ya kiutendaji.


Katika ziara yake katika Hospitali ya Mlele, Dk.Kigwangalla amewaagiza viongozi wa Serikali wa Wilaya na ule wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanakamilisha mambo muhimu ikiwemo ujenzi wa chumba cha upasuaji, jengo la kuhifadhia mahiti na vitu 
vingine huku akitaka ndani ya miezi mitatu view vimekamilika.


Akiwa katika Hospitali hiyo ya Mlele, Dk.Kigwangalla ameweza kutembelea sehemu mbalimbali za hospitali pamoja na kukagua ujenzi wa majengo ya Chumba cha upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti na majengo mengine ambapo amemtaka Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanafanya juhudi wanakamilisha kwa wakati majengo
 hayo ili wananchi wapate huduma bora.


Kwa upande wa ziara yake hiyo katika Wilaya ya Tanganyika yaliyopo makao makuu ya Mkoa wa Katavi, Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea Hospitali ya Mpanda ambayo
 kwa sasa inahudumia kama Hospitali ya Mkoa ambapo napo ameagiza kufanyiwa 
marekebisho mbalimbali ikiwemo kuzingatia masuala usafi.


Aidha, ametoa maagizo kuhakikisha wanafunga mfumo wa malipo wa kisasa katika
 vyanzo vyote vya mapato ili kukusanya pesa nyingi zaidi zitakazoweza kuendesha
 huduma  za Afya ndani ya Hospitali hiyo.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Chifu Kayamba wa Pili wa Kabila la Wakonongo. Wakati wa kupokelewa alipowasili ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mlele,Mkoani Katavi.

 Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bi.Rachel Kasanda akisoma taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati).

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya vifaa katika chumba cha Maabara ya hospitali ya Mlele.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link