Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro akipata maelezo .
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro katika picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Azimio,Kata ya Elerai.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Azimio,Kata ya Elerai.
SHULE YA AZIMIO YANUFAIKA NA TASAF III
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro ameweka jiwe la Msingi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe Mrisho Mashaka Gambo,
Mkuu wa Mkoa Mhe Mrisho Mashaka Gambo |
katika ujenzi unaoendelea wa vyumba viwili vya madarasa kwenye shule ya Msingi Azimio vinavyojengwa kupitia mradi wa Opec – Tasaf III.
Shule hii iliyopo kwenye Kata ya Elerai ilikua inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vitano vya madarasa ambapo iliwalazimu wanafunzi kusonagamana wakati wa masomo kwa kutumia vyumba vilivyopo.
Tasaf kwa kuliona hilo na kupitia miradi yake chini ya Opec ilianisha mradi huu wa ujenzi wa madarasa ili kukabiliana na changamoto zinazowakuta wanafunzi wakati wa masomo yao. Hivyo umeanza kutekezwa mwezi Agosti na utakamilika mwishoni mwa mwezi Novemba.
Akiweka jiwe la Msingi katika Shule hiyo Mkuu wa Wilaya Mhe. Daqarro amesema mradi huu wa Tasaf utakua wa manufaa kwa wanafunzi wa Azimio na bila shaka utaongeza uelewa na kuleta matokeo mazuri kwenye mitihani yao kwa sababu sasa adha ya msongamano itapungua.
Ujenzi wa madarsa hayo yatakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 90 na yatagharimu jumla ya sh Mil 70 huku Tasaf wakitoa Sh Mil 62.4 na wananchi wamechangia Sh Mil 7.6. Kazi hii itafanyika kwa muda wa miezi mitatu.
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.
03 Septemba,2016