WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa |
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amefanya mabadiliko ya uongozi kwa kumhamisha aliyekua Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHACO), Dk Musa Mgwatu kumhamishia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
Waziri Mbarawa amefanya mabadiliko hayo baada ya Rais Dk John Magufuli kuridhia mabadiliko hayo katika kuboresha utendaji.
Aidha Mbarawa amemteua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa kukaimu nafasi ya mtendaji RAHACO na ataendelea na wadhifa wake wa ukurugenzi wa TRL.