Home » » RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI WA KISIASA NA UTETEZI

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI WA KISIASA NA UTETEZI

Written By CCMdijitali on Friday, September 23, 2016 | September 23, 2016

 Na  Mwandishi Maalum, New York

Shirika lisilo la  Kiserikali    la Speak  Up for Afrika    limemtunukia tuzo, 
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na uongozi wake wa kisiasa na 
utetezi wake  kwa  makundi ya jamii  yaliyo katika mazingira magumu 
hususani wanawake na watoto.

Utoaji wa  Tuzo hiyo  ya  uongozi wa kisiasa na utetezi , umekwenda sambamba na   
hafla ya   miaka mitano ya kuanzishwa kwa  Taasisi ya Speak up  Afrika.
 Hafla  hiyo iliyofanyika  jana Alhamisi Jijini New York   ilikuwa  pia  ni sehemu ya kuhamasisha uchangiaji   wa shughuli za  Taasisi hiyo.

Mchango ambao umetambuliwa na  Speak Up  Afrika,   taasisi ambayo imekuwa ikifanya
 kazi  kwa Karibu na Rais Mstaafu Kikwete, ni  katika maeneo ya  upelekaji na 
usambazaji wa huduma za msingi za afya hususani afya ya mama na mtoto,  udhibiti wa 
 ugonjwa  wa malaria kupitia kampeni  ya malaria haikubaliki ,usambazaji wa vyandarua 
 vyenye viatilifu, kampeni ya  lishe bora, na  kampeni ya   chanjo kwa watoto.

Pamoja  na  kutambua  juhudi za   Rais Mstaafu  Kikwete katika  kuyasemea maeneo hayo,  Taasisi hiyo kupitia  Mkurugenzi wake  Mtendaji Bi. Kate Campana pia imemtambua  kama kiongozi ambaye    amekuwa mstari wa mbele  wa kulisema Bara la Afrika kila  mara alipopata  fursa  ya  kufanya hivyo wakati akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu.

Rais kikwete ameelezwa katika hafla hiyo iliyowashirikisha  wadau wa kada mbalimbali, kama kiongozi wa kisiasa ambaye amezigusa nyoyo za watu wengi kujitolea kwaajili ya watu wenye mahitajio ya kupata huduma za msingi za kijamii ambazo  au wameshindwa kuzipata
 kutokana na kipato kidogo au haziwafikii kabisa.

Akipokea  Tuzo hiyo, Rais  Mstaafu Kikwete , amesema Tuzo hiyo ni ya watoto wote  
waafrika ambao ndio  waliomfanya asimame   mbele ya wageni waalikwa.

“ Ni kwa sababu yenu ndio sababu nimetenga muda wangu  baada ya kustaafu kusukuma mbele agenda ya  kuboresha maisha yanu. Ninafanya hivyo kwasababu makuzi yangu yalikuwa kama 
 ya mtoto yeyote yule wa  kiafrika, nimeyaishi maisha  wanayo ishi. Na kwa hiyo ninaelewa
 fika  hamu na kiu yao ya kuwa  na maisha bora na afya njema”. 
Akasema Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.

Akaongeza kuwa  ,  mafaniko ambayo ameyapata katika  juhudi hizo  za kufikisha huduma za msingi  za kijamii kwa makundi  yenye mahitaji  yametokana na mambo mawili makubwa moja ni   aina ya uongozi  alioutumia kusukuma harakati hizo. Na pili  uhamasishaji uliofanyika katika  kupiga vita malaria kupitia Speak Up Afrika na    kampeni yao ya  malaria haikubaliki.

“ Nisingeweza kuyafanya niliyoyafanya   bila uungugwaji mkono na  ushirikiano  wa karibu nilioupata  na ninaoupata kutoka taasisi za kimataifa  ikiwamo hii ya  Speak Up  Afrika.
 Ndio maana  kwa mfano,  tumeweza kupunguza visa vya malaria kwa   theluthi mbilli,  tumefanikisha  upatikanaji wa chanjo kwa asilimia 96 kwa watoto wote na kupunguza vifo vitokanavyo na  malaria kwa   nusu.” Akaeleza Kikwete na kushangiliwa  tena.

Akasema, anamini katika ushirikiano na wadau mbalimbali  kama akina Ray Chambers kupitia kampeni ya  hakuna tena malaria, Taasisi ya  Bili na Melinda Gates na Gavi Vaccination   Alliance ambayo anashirikiano  nayo kwa karibu katika  kampeni ya chanjo kwa wote.

Rais  Mstaafu amewahakikishia   watendaji wa Speak  Up Afrika kwamba  ataendelea
 kufanya kazi nao kwa karibu  kutokana  kile alichosema amejionea
 mwenye kazi nzuri wanayoifana.

 Akawasihi  wadau mbalimbali  kuichangia taasisi hiyo  kwa kile alichosema, 
inafanya kazi kubwa  ya siyo tu kufikisha huduma za kijamii pale zinapotakiwa lakini  
pia imekuwa ni kipaza sauti cha Afrika.

Wengine waliopewa Tuzo kwa kutambua michango yao kwa jamii ni  pamoja na  
 Professa Awa Marie Coll- Seck, Waziri wa Afya  wa Senegal, Bibi Toyin  Saraki,  
mwanzilishi wa Taasisi ya  Wellbeing  Afrika ambayo  pia imekuwa ikitoa  elimu na
 misaada kwa wanawake na watoto pamoja na elimu  kwa wakunga na kutambua kazi nzuri,
 kubwa na ngumu  ya kuwahudumia wanawake wenzao wanapojifungua.  
Na  Bwana Kabirou Mbodje ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa  Taasisi ya  Wari.

Taasisi ya  Speak  Up  Afrika  imeanzishwa  na wanawake na inaongozwa na wanawake. 
Ni taasisi ambayo imejijengea uweo na sifa kubwa ndani  ya kipindi cha miaka 
mitano tangu  kuanzishwa kwake.   

 Rais  Mstaafu  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akipokea Tuzo ya  Uongozi wa Kisiasa na  Utetezi kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa  Speak Up Afrika  Bi Kate  Campana,  katika hafla iliyofanyika siku ya Alhamis  New York Marekani. Tuzo hiyo  ni kutambua jitihada na juhudi zake za kufikisha huduma za jamii hususani  afya kwa   kwa wanawake na watoto.

  Rais Mstaafu  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  baada ya  kupokea Tuzo yake akirejea kwenye kiti chake.


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza baada ya kukabidhiwa Tuzo yake na katika shukrani zake za kukubali Tuzo hiyo, amesema Tuzo hiyo ni kwa watoto wote wa Afrika ambao ndio wamemwezesha yeye kupata Tuzo
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link