ya Bahari na Maeneo Tengefu kulipa deni la sh. milioni 100 inayodaiwa na
Halmashauri ya wilaya ya Mafia.
Deni hilo linatokana na malimbikizo ya miaka mitatu ya maduhuri yatokanayo na makusanyo yanayofanywa na taasisi hiyo katika maeneo ya hifadhi ya bahari wilayani humo.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 23, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo katika ukumbi Caltas akiwa katika siku ya
kwanza ya ziara yake ya kikazi siku mbili.
“Waandikieni barua na muitume leo hii kwa njia ya mtandao (email) kuwajulisha kuwa wanatakiwa kulipa deni hilo ndani ya siku 10. Hakikisheni wanalipa deni hili ili
Halmashauri iweze kufanya kazi zake vizuri,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona Halmashauri hiyo ikinufaika kutokana na
vyanzo vyake vya mapato, hivyo haitakuwa tayari kuona ikihangaika.
Mbali na agizo hilo, Waziri Mkuun amesema atafuatilia kuona wajibu wa taasisi hiyo na
mipaka yao ikiwa ni pamoja na kujua mapato yatokanayo na shughuli hizo
katika maeneo ya hifadhi.
Awali mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alisema kuwa miongoni mwa
changamoto zinazoikabili wilaya hiyo ni kutolipwa kwa wakati fedha za maduhuri
yatokanayo na makusanyo yanayofanywa na Taasisi ya Hifadhi ya Bahari.
Mkuu huyo wa wilaya ameiomba Serikali kuangalia upya majukumu ya taasisi hiyo na
nafasi ya halmashauri katika kuendesha shughuli za uwekezaji pamoja na kupata
mapato yatokanayo na shughuli hizo katika maeneo ya hifadhi.