JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA RAISTAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAAHALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA | ||
Barua zote zitumwe kwa:
|
Mkurugenzi wa Jiji
| |
Simu:
Nukushi:
|
+255 27 2508073/2503494 (Director)
+255 27 2544330 (General)
+255 27 2545768
|
S. L. P. 3013,
20 Barabara ya Boma,
23101 ARUSHA,
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Tovuti: www.arushacc.go.tz
|
Unapojibu tafadhali taja:
| ||
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athumani J. Kihamia anawatangazi wazazi, walezi na wananchi wote wa Jiji la Arusha kwamba mitihani ya kumaliza elimu ya msingi itafanyika kuanzia tarehe 7-08/09/2016.
Kwa mwaka huu katika Jiji letu kuna jumla ya shule 111 zinazotarajiwa kufanya mitihani hiyo kati ya hizo 44 zinatumia mfumo wa Kiswahili na 67 zinatumia mfumo wa kingereza. Jumla ya watahiniwa wote ni 9992 kati ya hao 7239 wanatoka kwenye shule zinazofundisha kwa mfumo wa Kiswahili na kati yao wavulana ni 3,424 na wasichana ni 3,815. Idadi ya watahiniwa wa mfumo wa kingereza ni 2,753 kati ya hao wavulana ni 1371 na wasichana ni 1,382.
Mkurugenzi wa Jiji anapenda kuwatakia kila la kheri watahiniwa wote na kuwataka kuwa watulivu kwa kipindi chote cha mitihani na kufuata taratibu na maelekezo ya wasimamizi.
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.
06 Septemba,2016