Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua, akisoma tamko la Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Arusha,mbele ya vyombo vya habari Ofisini kwake ,Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha,Septemba 26,2016.
Picha ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Arusha,mara baada ya Kikao ,Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli (aliyevaa shati la kijani) MNEC Ndg Godfrey Mwalusamba (aliyevaa koti ,wa pili kutoka kushoto) mkuu wa Wilaya ya Arusha Ndg Gabrelly Daqarro (aliyeshika diary )Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya Ndg Jasper Kishumbua (mwisho kushoto) Bi Halima Mamuya , Ndg Ally Mtumwa (aliyekaa nyuma kabisa) na Ndg Martin Munisi (mwisho kulia) wakiwa nnje ya Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Septemba 26, 2016.
Picha ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Arusha,mara baada ya Kikao ,Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli (aliyevaa shati la kijani) MNEC Ndg Godfrey Mwalusamba (aliyevaa koti ,wa pili kutoka kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Arusha na Mjumbe Ndg Gabrelly Daqarro (aliyeshika diary )Katibu wa CCM Wilaya Ndg Feruzzy Bano (aliyekaa nyuma kabisa) Bi Halima Mamuya , Ndg Ally Mtumwa (mwisho kushoto) wakiwa nnje ya Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Septemba 26, 2016.
NA
SHAABAN MDOE,ARUSHA.
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Arusha kimempongeza mwenyekiti wake taifa ambaye
pia ni Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli na serikali
yake kwa utendaji wake mzuri na wenye kutia matumaini tangu alipochaguliwa
mnamo Oktoba 25 mwaka jana 2015.
Akisoma
tamko rasmi la kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Arusha
katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Arusha Jasper Kishumbua alisema kikao hicho
kilichoketi Septemba 24 mwaka huu pamoja na mambo mengine ikiwemo musatakabali
wa chama pia kilitoa pongezi hizo.
Katika
tamko hilo Kishumbua aliyataja mambo machache yaliyofanywa na Rasi Magufuli
katika wakati wake wa uongozi kuwa ni pamoja na Kurudisha nidhamu ya utendaji
kazi kwa watumishi Serekalini.
Mengine
kuongeza mapato ya serikali kutokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo kodi kutoka
shilingi milioni 900 kwa mwezi hadi kufikia shilingi trilioni 1.04 kwa mwezi
baada ya kuingia maarakani.
Aidha
alisema kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Arusha
inafurahishwa na utekelezaji wa ahadi zake
ambazo amekuwa akizitoa kwa nyakati tofauti ikiwemo ya kuipatia idara ya
mahakama fedha za kuendeshea shughuli zao na kuboreshe mhimili huo wa serikali.
Pia
ilipongeza hatua za Rais Magufuli za kulifufua upya shirika la ndege la Taifa
(ATCL) ambapo hivi karibuni tumeshuhudia ndege moja kati ya tatu alizoahidi
zikiwasili nchini jambo litakalorahisisha usafiri wa anga hapa nchini.
“Ndugu
zangu haya yote yanatudhihrishia wazi kuwa tumepata Rais wa ndoto yetu sisi
watanzania kikao chetu kinampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuanza kurejesha
uhai wa shirika hili muhimu la serikali na lenye huduma nafuu kwa Watanzania wa
kawaida”alisema Kishumbua.
Aidha
kupitia kikao hicho kwa upande mwingine Kamati hiyo ilimpongeza MKuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro pamoja na
timu zao,kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama
cha Mapinduzi.
Viongozi
hawa wamekuwa mstari wa mbele kutatua matatizo na kero za wananchi wa jiji la
Arusha ambayo kwa kipindi kirefu sasa yamekuwa hayapatiwi ufumbuzi ikiwemo malipo
ya malimbikizo ya walimu yaliyofikia kiasi cha shilingi Milioni 169 yaliyoweza
kulipwa kutokana na kuzuiwa kwa posho za nje ya utaratibu kwa madiwani wa jiji.
Aidha
kikao hicho kimekemea kwa kauli moja tamko lisilo na tija na lilojaa uchochezi
kwa wananchi dhidi ya serikali na viongozi wao lililotolewa na Mstahiki Meya wa
Jiji la Arusha Kalist Lazaro kwamba serikali ya wilaya na mkoa inakiuka
taratibu za uongozi kwa kuingilia uendeshaji wa halmashauri ya jiji.
Hata hivyo
kikao hicho kiliwasihi wanawasihi,Viongozi
wa Kisiasa na wa Taasisi nyingine,wenye mapenzi mema na nchi kuache mara moja
kutoa matamko yenye mrengo wa kiharakati ili kufifisha jitihada zinazofanywa na
Serikali za kutatua matatizo ya wananchi kuelekea kwenye maendeleo ya kweli ya
viwanda.
Mwisho.
TAMKO LA KAMATI YA
SIASA YA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA ARUSHA KUHUSU UTENDAJI KAZI WA
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
24 SEPTEMBA 2016.