![]() |
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa |
mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Kwa ufupi
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa matapeli hao huzisambaza barua hizo kwa kampuni binafsi na wakuruegnzi watendaji wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya ‘Mkutano Mkuu wa Rekebisho la Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia Septemba 21 hadi 23, mwaka huu.
Dar es Salaam. Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imewatahadharisha Watanzania kuhusu kuwapo kwa matapeli wanaotumia nembo ya ofisi hiyo na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, kuchapisha na kusambaza barua kisha kuchangisha fedha.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa matapeli hao huzisambaza barua hizo kwa kampuni binafsi na wakuruegnzi watendaji wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya ‘Mkutano Mkuu wa Rekebisho la Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia Septemba 21 hadi 23, mwaka huu.
“Mnataarifiwa kuwa barua hizo zilizotiwa saini na zenye muhuri wa kughushi huku maelezo yake yakiwa hayaeleweki vizuri, hazijaandikwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, bali zimeandikwa na watu wenye nia mbaya na wanaolenga kujipatia fedha kwa njia ya utapeli,” ilimesema taarifa hiyo iliyotolewa sainiwa na Msigwa.