CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO

  Na Richard Mwaikenda, Mwanza   Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwa...

Latest Post

Uzinduzi wa Kliniki ya Tiba Mtandao, Shule Direct pamoja na Kituo cha kuhifadhi Utamaduni wa Kimaasai - ARUSHA

Written By CCMdijitali on Monday, October 31, 2016 | October 31, 2016

 Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Rashid Taka akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto aliyeketi) kuhutubia wageni waalikwa na wanakijiji wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa kijiji cha kidigitali chenye kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Arusha.

 
 Pichani juu na chini ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akisoma hotuba katika hafla ya uzinduzi wa kijiji cha kidigitali chenye kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu uliofanyika kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Pichani juu na chini ni baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan na wageni waalikwa  wakimsikiliza mgeni rasmi RC Gambo kwenye hafla ya uzinduzi wa kijiji cha kidigitali chenye kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao uliofanyika mwishoni mwa wiki, wilayani Simanjro, mkoani Arusha.


 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akizungumzia ukuaji wa teknolojia ambayo inaenda sambamba na maono ya shirika lake kwenye hafla uzinduzi wa kijiji cha kidigitali chenye kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao uliofanyika mwishoni mwa wiki, wilayani Simanjro, mkoani Arusha.


 Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori akizungumza kwenye hafla uzinduzi wa kijiji cha kidigitali cha Samsung (Samsung Digital Village) kinachotumia umeme wa jua chenye kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao uliofanyika mwishoni mwa wiki, wilayani Simanjro, mkoani Arusha.

Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli akizungumza kwenye uzinduzi wa kijiji cha kidigitali cha Samsung (Samsung Digital Village) kinachotumia umeme wa jua ambacho kina kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kilichopo katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Simanjro mkoani Arusha.
 
 Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Dr. Margaret Mhando akitoa neno ambapo aliwashukuru Unesco kusaidia kutekeleza malengo ya wizara kupitia mradi huu wa kijiji cha kidigitali cha (Samsung Digital Village) unaoratibiwa na Shirika la UNESCO kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akimsikiliza kwa makini Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli wakati wa hafla ya uzinduzi wa kijiji cha kidigital cha Samsung chenye kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao (Samsung Digital Village) uliofanyika kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akijipanga kuzindua rasmi moja ya kituo cha huduma maalum za afya huku Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori (katikati) Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli (kushoto), Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Dr. Margaret Mhando (kulia), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) wakishuhudia tukio hilo.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akikata utepe kuzindua rasmi moja ya kituo cha huduma maalum za afya huku Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori (katikati) Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli (wa pili kushoto), aibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao (kushoto), Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Dr. Margaret Mhando (kulia), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) wakishuhudia tukio hilo.

 Mganga Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari akitoa maelezo ya huduma mbalimbali za Afya zitakazokuwa zikipatikana ndani ya moja ya makontena ya kijiji cha Kidigitali cha Samsung (Samsung Digital Village) kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma maalum za afya uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akifanya kipimo cha B.M.I ndani ya kituo cha huduma maalum za afya kilichopo katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha mara baada ya kukizundua rasmi.

 Mganga Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari akimsoea majibu ya BMI Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ndani ya kituo cha huduma maalum za afya kilichopo katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha ambacho kimezinduliwa rasmi mwishoni mwa juma.

 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) akifurahi jambo wakati Mganga Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari (katikati) akimsoma majibu ya BMI Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia) akiwa ndani ya Kliniki hiyo ya Kidigitali ya Samsung akifanya uchunguzi wa kupima uwezo wake wa kusikia kwa kutumia kifaa maalum.

 Mratibu wa Telemedicine kutoka Wizara wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dk. Liggy Vumilia akifafanua kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (hayupo pichani) jinsi kituo cha huduma maalum za afya cha kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kinavyoweza kufanya mawasiliano na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa njia ya mtandao na kupata ufumbuzi wa tatizo la mgonjwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho. Kulia ni Stella Kairuki kutoka Samsung.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akitoa mkono wa pongezi kwa Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori kwa kusogeza huduma muhimu za afya kwa wanakijiji wa Ololosokwan mara baada ya kuzindua kituo hicho cha afya wilayani Ngorongoro mwishoni mwa juma.

 Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akimpongeza Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues kwa kuratibu mradi huo utakaowasaidia wanakijiji wa Ololosokwan katika huduma za afya na elimu kwa njia ya mtandao.

 Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao, Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori pamoja na Afisa Utawala na Fedha wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Spencer Bokosha wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha huduma maalum za afya uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Televisheni ya Samsung iliyopo nje ya kituo hicho cha huduma za afya ikionyesha kipindi maalum cha kuelimisha jamii ya wafugaji (Wamasai) wa kijiji cha Ololosokwan iliyotafsiriwa Kimasai kuhusiana na masuala ya afya na usafi wakati wakisubiri kupata huduma za afya.

 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa wageni waalikwa nje ya kituo cha huduma ya meno na maabara ya kijiji cha kidigitali wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao (Samsung Digital Village) uliofanyika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akibadilishana mawazo na Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha huduma maalum za afya uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenye picha ya pamoja na wadau waliofanikisha mradi wa Samsung Digital Village pamoja na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan watakaonufaika na mradi huo.

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori (kushoto) Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Dkt Moshi Kimizi (wa pili kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao (kulia) wakiwasili kwenye eneo la kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kwa ajili ya uzinduzi rasmi katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. 
Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na Wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Olivier Couplex (wa pili kulia) pamoja na Anna Costantine wakiwasili ene la tukio.

 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues na Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli wakifurahia jambo kwenye hafla ya uzinduzi huo.

 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akikaribishwa kwa ngoma za kimasai katika eneo la tukio.

 Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori akizungumza machache jengo la kituo cha elimu kwa njia ya mtandao ambalo limetengenezwa na Samsung kabla halijazinduliwa rasmi kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akitoa neno wakati wa jengo la kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kabla kuzinduliwa rasmi kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kinachotumia umeme wa jua (Solar Power Internet School) uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori (wa tatu kushoto) Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao (wapili kushoto), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia).

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Emanyata ya Loliondo, Kenneth Pascal wa kidato cha pili akitoa elimu kwa njia ya mtandao kupita programu ya Shule Direct kwa wanafunzi wenzake wa darasa la kompyuta waliojumuika na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati wa sherehe ya uzinduzi wa kituo hicho uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, Wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati), Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao wakiwa ndani ya kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kinachotumia umeme wa jua (Solar Power Internet School) mara baada ya kukizindua katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Darasa la kompyuta kwa njia mtandao likiendelea huku wageni wakishuhudia.

 
 Mafunzo kwa vitendo yakiendelea.

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akifuatilia kwa makini darasa lililokuwa likiendeshwa na mwanafunzi wa kidato cha pili (hayupo pichani).

ARUSHA - Wananchi wa Mundarara wajitolea ujenzi wa Daraja

Written By CCMdijitali on Sunday, October 30, 2016 | October 30, 2016



 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyeko kwenye mtaro) akishiriki ujenzi wa daraja la chini linalojengwa na wananchi wa Mundarara.



 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akimkabdihi Mkuu wa Shule ya Sekondari  Engaranaibo  Mwl. Petro Sabatho Tsh 500,000 kwa ajili ya  kuchangia ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule hiyo wakati wa ziara yake inayoendelea katika Wilaya ya Longido.



 Viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Arusha pamoja na wananchi wa kijiji cha Olgira Kata ya Mundarara wakielekea kwenye eneo la ujenzi wa daraja ambalo linajengwa kwa nguvu za wananchi.




 Hili ndilo daraja ambalo wananchi wa Kata ya Mundarara wamejitolea fedha na nguvu zao kuhakikisha ujenzi wa daraja unakamilika na kufanya barabara zinazounganisha vijiji vyao kupitika kipindi chote cha mwaka.



 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akihamasisha wananchi waendelee kuchangia ujenzi wa daraja la Mundarara ili liweze kukamilika kwa wakati.




 Wanawake wa Jamii ya Kimaasai maarufu kama Siangiki walijitokeza barabarani kumlaki Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara yake wilayani Longido.


Mabinti wa jamii ya kimaasai maarufu kama Selengeni pia walishirki mapokezi ya Mkuu wa Mkoa wakati wa ziara ya kazi wilayani Longido.

Nteghenjwa Hosseah - Longido
 

Wananchi wa Kijiji cha Orgirah Kilichopo Kata ya Mundarara Tarafa ya Engarenaibor Wilayani Longido wamelazimika kutumia nguvu zao binafsi kujenga daraja la chini kwa ajili lengo la kuunganisha mawasiliano ya barabara kati ya kata hiyo na kata ya Gelai.

Aidha wamelalamikia kero ya maji tangu mwaka 2013 hadi leo hii hakuna maji yanayotoka kwenye mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) unaolenga kusaidia vijiji vitano kwenye kata hiyo.

Wakiongea na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye anaendelea na ziara yake kwenye wilaya hiyo jana, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Orgirah, Mathayo Laizer alisema mradi huo wa daraja ni muhimu kwao kwani unafungua fursa za kimaendeleo katika kata mbili za Mundarara na Gelai.

Alisema mradi ulianza mwaka jana na walipata michango mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo  ambayo ilitoa Sh. 400,000, Ofisi ya Mkurugenzi Sh, 640,000 na wananchi walichanga Sh, milioni 5.3 lakini ili waweze kukamilisha ujenzi wa daraja hilo wanahitaji mifuko ya saruji 135 pamoja na ndono za kuweka kingo pembeni ya daraja hilo zenye thamani ya Sh milioni 2.9

Naye Esther Mathayo alimuomba Rc, Gambo kuwasaidia kutatua kero ya maji katika kata hiyo ambayo ipo kwenye mradi wa benki ya Dunia tangu mwaka 2013 lakini hadi leo wananchi wanatembea umbali mrefu kutafuta maji hayo kwaajili ya matumizi mbalimbali.

Alisema awali mradi huo uliofadhiliwa na benki ya dunia ulilenga kusaidia vijiji vitano na ulijengwa katika kata hiyo zaidi ya miaka minne iliyopita lakini cha ajabu kwenye chanzo cha maji hakukuguswa na baadhi ya miundombinu imeharibika iliyokwisha wekwa awali sehemu mbalimbali na hawajui ni kwanini umekwama.

Baada ya wananchi kutoa kero zao, Rc Gambo aliwapongeza wananchi hao kwa ujenzi wa daraja hilo la chini kwa kutumia nguvu zao wenyewe kwa kuleta maendeleo ikiwemo kufungua njia za mawasiliano kati ya sehemu moja na nyingine.

"Nawapongeza kwa kazi hii mliyojitolea kwaajili ya kutatua changamoto ya usafiri lakini pia natoa rai kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido, Juma Mhina kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa mradi huu wa maji kama ni fedha watenge kwenye bajeti ya halmashauri hiyo ili wananchi wanywe maji "

Pia aliweza kuchangia mifuko ya saruji 30, pamoja na kufanya harambee na kuchangisha zaidi ya Sh, milioni 1 kutoka kwa watumishi wa sekta mbalimbali alioambatana nao ili daraja hilo liweze kukamilika,awali Gambo kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya hiyo, Daniel Chongolo waliingia ndani ya kingo za daraja hilo kwaajili ya kusaidiana na wananchi kuweka mawe kwenye msingi wa daraja pamoja na wananchi wa kijiji hicho.


Mwisho





ARUSHA - Mtendaji wa Kata aswekwa Rumande kwa Matumizi mabaya ya Fedha za Umma



 Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakionyesha  zana  walizotumia kutengeneza barabara  ya Km 24 kwa nguvu zao wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo  katika  Kijiji hicho.




 Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakishangilia Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ulipokuwa unawasili katika Kijiji hicho.



 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Mbele kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo(Mbele  Kulia) wakiwasili  kwenye Mkutano wa hadhara  katika Kijiji cha  Esokonoi.



 Mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa Arusha  Mhe. Michael Lekule Laizer akiongea na wananchi wa Kijiji cha  Esokonoi wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Wilaya hiyo.




 Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi wakimskilizia Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo (hayupo pichani) alipokua akizungumza nao kwenye Mkutano wa hadhara.



 Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mhe. Michael Lekule Laizer(kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  (Katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido wakiwa katika mavazi ya asili ya Kimasaai waliyovishwa kwa heshima na wananchi wa Esokonoi.



Watoto wa Jamii ya Kimasaai pia walihudhuria Mkutano wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika Wilaya ya Longido.


Nteghenjwa Hosseah – Longido


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Londifo, Juma Mhina ameamuru polisi wa Wilaya hiyo kumkamata na kumuweka ndani  Mtendaji wa Kata ya Gilai Lumbwa, Paul Lucas baada ya kutuhumiwa kutumia Fedha za umma vibaya zilizochangwa na wananchi wa maeneo hayo kwa ajili ya kuinua Sekta ya Elimu.

Agizo hilo la Mhina lilifanikiwa baada ya mara kwa mara kushindwa kumkamata Paulo baada ya kumkwepa kila alipokuwa akitafutwa na hatimaye mtendaji huyo kujitokeza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisgo Gambo uliofanyika kwenye Kijiji cha IIchang Sapukin kata ya Gilailumbwa.

Mmoja kati ya wananchi walioshirki Mkutano huo Bi. Anni Mollel alimshukuru Rc Gambo kufika Kijijini hapo na kujionea hali halisi ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ambayo wananchi walichanga Fedha zao zaidi ya Tsh Mil 96 ila hazikutumika kama ilivyokusudiwa badala yake viongozi wa Serikali na Wenyeviti wa Kijiji walitumia Fedha hizo kujinufaisha binafsi badala ya kuwasaidia watoto kukaa kwenye mazingira mazuri ili wapate Elimu.

“Yaan bora umekuja Mkuu hawa viongozi wetu huku kijijini ni Miungu watu wanajipangia mambo yao ya kubadilisha matumizi ya Fedha  zilizochangwa na wananchi kaka zao yaan ukiwaangalia wao wana maisha mazuri wakati sisi tunateseka sasa lro uondoke nao na tunamuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hii Ndg. Mhina kuwaleta watumishi wengine na wale waliohamishwa hapa baada ya kushirki kula hela zetu wakamatwe pia na waseme wamepeleka wapi hela zetu”

Mara baada ya wananchi kusema hayo Gambo alimhoji Mkurugenzi Mhina ni kwa nini hawajachukua hatua za kisheria  kuwakamata watuhumiwa ndipo Mhina aliposema  mbele ya hadhara hiyo kwamba zoezi hilo lilishindikana awali baada ya Paulo kumkwepa Mkurugenzi huyo mara kwa mara lakini jana alijileta mwenyewe katika mkutano huo  na ndipo imekuwa rahisi kwake kumkamata.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmahauri hiyo, Bi. Mwajuma Mndaira kwenye  Mkutano huo alidai kuwa alifanya mahojiano na wenyeviti wa vijiji kujua ni kwa nini walikusanya Fedha kwa wananchi bila kutumia stakabadhi za Serikali katika zoezi hilo.

Pia hivi sasa bado wananendelea na uchunguzi wa nyaraka za malalamiko mbalimbali ili kubaini Paulo alihusika na kinanani na kwa nini abadilishe baadhi ya matumizi ya Fedha hizo na kuuza  baadhi ya vitu vilivyochangwa bila kuonyesha sababu ya Msingi kwani baadhi ya kampuni za uwindaji wa kitalii ikiwemo Wingert WindroseSafaris na Kampuni ya Kilombero Nothern Safaris zilitoa mifuko ya Saruji 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari hiyo.

Rc Gambo alimuhoji Mtendaji huyo kwanini shule hiyo haijakamilika  mpaka leo wakati  watoto wa jamii ya kifugaji wana haki ya Kupata Elimu na wazazi wao wanajitoa wa ajili ya watoto wao huku yeye akiendelea kuwarudisha nyuma, Paulo alijitetea kwamba baadhi ya fedha hizo ziliztumika kihalali na fedha zingine alilazimik kubadilisha matumizi yake na kujenga vyumba vya maabara, jiko pamoja na mabweni.

Baada ya utetezi wake kugonga mwamba alijikuta yupo chini ya himaya ya Polisi waliokuwa wakiongoza msafara huo ambapo pia Mkuu wa Wilaya hiyo Chongolo aliahidi wananchi hao kuwa atafuatilia suala la watumishi  wengine watakoziba nafasi za wote watakaomatwa na ubadhirifu huu kuletwa haraka iwezekanavyo ili huduma zisizorote na endapo tuhuma hizi zikithibitkka watapelekwa Mahakamani  na aliongezwa kuwa atakua karibu nao kuhakikisha kero kama hizo hazijitokezi rena hapo baadae .

Mwisho




 


 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link