Home » » Kesi ya ubunge wa Longido bado mbichi

Kesi ya ubunge wa Longido bado mbichi

Written By CCMdijitali on Monday, October 24, 2016 | October 24, 2016



 Jengo la Mahakama Kuu ya Mkoa wa Arusha.

 Katibu wa UWT Mkoa wa Arusha Bi Fatuma Tsea,akitoka Mahakamani.

 Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg Omari Bilali (aliyevaa miwani ) akiongea na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Arusha Ndg Shaabani Mdoe,mara baada ya kesi kusogezwa mbele.


 Mbunge wa Jimbo la Arusha Ndg Lema ,Mkewe na Onesmo Nangole wakiteta jambo mara baada ya kesi kuahirishwa,nje ya jengo la Mahakama.

 Mwanasheria Ngemela  (mwenye joho kushoto) mara baada ya kesi kuahirishwa ,chini kabisa mwenye shati la drafti ni Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Ndg Mussa Juma,akipata habari kutoka kwa Mawakili wanaomtetea Ndg Onesmo.


Baadhi ya Viongozi wa CCM Wilaya ya Arusha wakiteta jambo mara baada ya kusogezwa mbele.


Kwa ufupi

Lengo la kusogeza mbele ni kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Msimamizi wa Uchaguzi.


Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imesogeza mbele kusikiliza hukumu ya rufani ya kesi ya ubunge wa Longido.

Lengo la kusogeza mbele ni kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Msimamizi wa Uchaguzi.

Majaji wa Mahakama ya Rufani, Sauda Mjasiri, Mussa Kipenka na Profesa Ibrahim Juma wametoa uamuzi huo jana uliosomwa na Msajili wa Mahakama, John Kahyoza.

Katika maamuzi hayo, aliyekuwa Mbunge wa Longido (Chadema), Onesmo ole Nangole anayepinga matokeo kutenguliwa, alitakiwa kuwaongeza ndani ya siku 21, AG na Msimamizi wa Uchaguzi kwa kuwa ni muhimu katika kesi hiyo ili kuendelea na rufani ya msingi.



By Mussa Juma na Moses Mashalla, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link