Home » » Maghembe: Udokozi unawaponza Watanzania

Maghembe: Udokozi unawaponza Watanzania

Written By CCMdijitali on Wednesday, October 19, 2016 | October 19, 2016

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe

Kwa ufupi

Akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Maghembe amesema kazi za hoteli zinahitaji watu waaminifu.


Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema tabia ya udokozi ni miongoni mwa sababu ambazo zinazowafanya wenye hoteli wapende kuajiri wageni badala ya watanzania.

Akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Maghembe amesema kazi za hoteli zinahitaji watu waaminifu.

Amesema wageni wanapofika na kupanga kwenye hoteli zetu wanahitaji Huduma bora na usalama wa mali zao.

"Lakini wabongo wengi ni wapigaji (wezi) hali ambayo huharibu taswira ya hoteli nyingi"amesema.

Profesa Maghembe amesema matokeo yake wageni wakiibiwa hawawezi kurudi tena kwenye hoteli hizo. Ametoa wito kwa uongozi wa chuo hicho kufundisha uaminifu katika kazi.

By Raymond Kaminyoge, Mwananchi

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link