Home » , » MFALME MOHAMED VI KUTOKA TAIFA LA MOROCCO AWASILI JIJINI DAR JIONI HII,APOKELEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT MAGUFULI

MFALME MOHAMED VI KUTOKA TAIFA LA MOROCCO AWASILI JIJINI DAR JIONI HII,APOKELEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT MAGUFULI

Written By CCMdijitali on Sunday, October 23, 2016 | October 23, 2016


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake,Mfalme Mohamed VI kutoka Taifa la Morocco wakipata Gwaride la heshima,mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar jioni hii.

 Pichani ndege aina ya Boeing 747 iliyombeba Mfalme Mohamed VI wa Morocco na ujumbe wake ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jioni hii jijini Dar na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

 Sehemu ya ujumbe alioongozana nae Mfalme Mohamed VI kutoka Taifa la Morocco,aliyewasili jioni ya leo na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake,Mfalme Mohamed VI kutoka Taifa la Morocco wakipata Gwaride la heshima,mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar jioni hii.Mfalme huyo amewasili jioni ya leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu,aidha imeelezwa kuwa Mfalme huyo aliyekuja na ujumbe wa watu takribani 1000,mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu,atakuwa na siku nyingine tano za mapumziko hapa nchini ambapo atatembelea maeneo mbalimbali ya vivutio na utalii nchini Tanzania


Video »







Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link