Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA MKUU WA MKOA ARUSHA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo leo ametekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli la kusitisha safari ya kwenda Mkoani Simiyu kwenye sherehe za kuhitimisha kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa kurejesha Fedha kiasi cha jumla ya Shilingi 1,389,300 ambayo yalikua ni malipo halali kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa, msaidizi, dereva pamoja na gharama za mafuta.
Wakati agizo hilo linatolewa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Arusha alikua bado hajaanza safari ya kuelekea Mkoani Simiyu ingawa taratibu zote za safari zilikua zimekamika.
Aidha Rc Gambo ameanza kusimamia wahusika wote Mkoani hapa waliokwisha pokea fedha kwa ajili ya safari hiyo ili kuhakikisha wanatekeleza agizo la Mhe. Rais kwa wakati na Fedha zitakazookolewa zitaelekezwa kwenye ujenzi wa madarasa kama sehemu ya maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, darasa la kwanza na darasa la awali kwa mwaka 2017.
Imetolewa na:
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari