Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha
Jeshi la Mkoani Arusha linawashikilia watu wanne akiwemo mmiliki wa Kambi ya LILAC inayojishulisha na maswala ya utalii, Mtowambu, John Kadozo(46) mwenye asili ya kiasia mkazi wa Mtowambu wilayani Monduli kwa tumuma za kumuunguza kwa kumwagia petroli mfanyakazi wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea October 9 saa nne Usiku ndani ya Kambi ya mtuhumiwa iliopo Mtowa mbu wilayani Monduli.
Alisema kuwa mtumiwa alimchoma moto mtoto aliyejulika kwa jina la Paskali Alfonce (17) mkazi wa Mtowambu aliyekuwa mpishi wa kampuni yake kwa kumtuhumu kuchelewa kupika maharage.
"Inasemakana kijana huyu alikuwa mpishi wa pale sasa Siku hiyo alipewa fedha akanunue maharage alipoenda alichelewa kurudi ndipo mtuhumiwa na wenzake walipomkamata kijana huyo na kumwagia petroli kisha kumuwasha moto "alisema Mkumbo
Aliwataja watuhumiwa wengine ambao wanatuhumiwa kuhusika na tukio hilo ambao pia wanashikiliwa na polisi kuwa ni John Kadozo (46), George Kessy (28), Martin Petro (16), Enock Wilium (19) na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema iwezekanavyo .
Akisimulia tukio niko kwa uchungu mtoto Alfonce ambaye amelazwa katika hospitali Seliani iliopo ngaramtoni alisema siku hiyo alitumwa maharage ila alichelewa kurudi kutokana na kuyakosa lakini aliporudi ndipo walipomkamata na kumfunga shuka mikono wakamwagia petroli kisha kumchoma.
"Nilibahatika kuchoropoka nikakimbia sasa Jirani name apo kunamfereji nika rukia uko ndio nikazimika maana niliwaka kabisa "alisema mtoto Alfonce
Akilia kwa uchungu mama mlezi aliyejitambulisha kwa jina la Cristina Faustine alisema anasikitika sana maana AME Lea uyo toto kwa shida tangu wazazi wake wafariki na aliamua amruhusu kwenda kufanya kazi ili aweze kujikimu na aweze kujipatia maitaji yake.
Aidha alitumia muda huo kuiomba serekali kuhakikisha mtoto huyo anapata matibabu na kwani kwasasa anauwezo wa kugaramia matibabu ya huyo mtoto.
Na Woinde Shizza, Monduli