Home » » Viongozi wa CCM Kata watembelea Ofisi ya Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Arusha.

Viongozi wa CCM Kata watembelea Ofisi ya Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Arusha.

Written By CCMdijitali on Friday, October 7, 2016 | October 07, 2016

Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lemara Ndg Emmanuel Betuel,Katibu wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Jane Nyari ,Katibu wa UWT Kata ya Sinoni Bi Mariamu Ramadhani na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Sinoni Bi Sophia Ally,wakiwa katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.


Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lemara Ndg Emmanuel Betuel,Katibu wa WAZAZI Wilaya ya Arusha Ndg Mohamed Mavallah ,Katibu wa UWT Kata ya Sinoni Bi Mariamu Ramadhani na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Sinoni Bi Sophia Ally,wakiwa katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.


 Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Sinoni Bi Sophia Ally,Katibu wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Jane Nyari na Katibu wa UWT Kata ya Sinoni Bi Mariamu Ramadhani na ,wakiwa katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lemara Ndg Emmanuel Betuel,akiwa katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.



 Katibu wa UVCCM Kata ya Kaloleni Bi Lucy Sixtusy na Katibu wa UVCCM Kata ya Kati Bi Jamila Male  ,wakiwa katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.


 Katibu wa UVCCM Kata ya Ngarenaro Bi Arafa Mussa na Katibu wa UVCCM Kata ya Levolosi Bi Fatuma Abdallah ,wakiwa katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.


Press Release:-


Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha
Leo tarehe 7 Septemba, 2016 viongozi wa CCM kutoka kata mbalimbali za Wilaya ya Arusha wametembelea ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi ya CCM Wilaya ya Arusha na kukutana na Ndugu Jasper Kishumbua Katibu wa idara hiyo muhimu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya.     


Wakiwa Wilayani hapo viongozi hao toka Kata walibadilishana mawazo juu ya mwenendo mzima wa siasa za Wilaya ya Arusha kwa upande wa CCM na Jumuiya zake. Wakiwa na bashasha na matumaini tele, wote kwa pamoja wakiongozwa na Katibu Mwenezi Ndugu Jasper Kishumbua na Makatibu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Mohamed Mavallah na UWT Bi Jane Nnyari walikubaliana kuwa silaha pekee itakayotuongoza katika kuiimarisha CCM na Jumuiya zake kuelekea Chaguzi za mwaka 2019 na  2020 ni UMOJA.


Pamoja na yote katibu wa Siasa na Uenezi alihimiza na kusisitiza kuwa kila ngazi ya uongozi ya Chama na Jumuiya zake kufuata Kalenda ya Vikao Vya Chama Cha Mapinduzi 2016 na kusimamia yale yote yaliyohimizwa kama AGENDA ZA KUDUMU kwa kuwa haya ndiyo yatakuwa maandalizi bora zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa CCM na Jumuiya zake unaotakiwa kufanyika Mwakani 2017.


CCM OYEEE ! 

UMOJA NI USHINDI!





Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link