Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Uganda waliokuja kujifunza masuala ya kiutumishi nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Uganda Mhe. Jacob Oboth-Oboth (kulia) alipotembelewa na kamati hiyo Ofisini kwake kwa ajili ya kujifunza masuala ya kiutumishi.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama akitoa ufafanuzi wa masuala ya maadili katika Utumishi wa Umma kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Uganda waliokuja kujifunza masuala ya kiutumishi nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya moja na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Uganda waliokuja nchini kujifunza masuala ya kiutumishi. Kushoto kwake ni
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiagana na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Uganda mara baada ya kumaliza mazungumzo na wajumbe hao waliokuja nchini kujifunza masuala ya kiutumishi.