Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(katikati) akiwasili kwenye Machinjio ya Manyara Ranch kukagua mradi huo uliopata fedha za wafadhili zaidi ya Tsh Mil 400.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kati mbele) akipokea taarifa ya Machinjio ya Manyara Ranch toka kwa Meneja wa AWF Ndg. Fidelisi Ole Kashe(mbele)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya ya Monduli baada ya kubaini ubadhirifu wa Fedha katika wa Mradi wa Machinjio.
Muonekano wa Machinjio ya Manyara Ranch
Malaigwanani wa Kimaasai Wilayani Monduli wakimsimika Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyekaa kwenye Kigoda) kuwa Laigwanani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Esilalei.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kushoto), Mbunge wa Monduli Mhe. Julius Kalanga pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mhe. Isack Joseph kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Esilalei.
Nteghenjwa Hosseah, Monduli
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na
Rushwa Mkoani Arusha (TAKUKURU) kuhakikisha inawakamata na kuwafikisha
mahakamani wale wote waliokula fedha zaidi ya shilingi milioni 448.9 za maradi
wa machinjio uliopo ndani ya shamba la Manyara Ranch lililopo wilayani Monduli
Mkoani Arusha.
Gambo
alisema hayo mara baada ya kutembelea machinjio hayo ya kisasa yaliyopo ndani
ya shamba hilo la ekari 44,930 na kuelezwa kuwa mradi huo ulianza mwaka 2009 na
hadi sasa ulikuwa haujamalizika.
Alisema
inasikitisha kuona mradi toka mwaka 2009 zaidi ya miaka saba haujakamilika
pamoja na kwamba fedha zaidi ya shilingi milioni 448.9 zilitolewa ikiwa ni gharama
za ujenzi na ujenzi wa jengo la machinjio uligharimu zaidi ya shilingi milioni
223.5 na ununuzi wa vifaa vingine vya kisasa kwa ajili ya machinjio zilitolewa
zaidi ya shilingi milioni 225.4
Mkuu
huyo alisema kuwa fedha zimetolewa na wafadhili ambao ni USAID kupitia shirika
la African Wildlife Foundation{AWF} lakini zimeliwa na wajanja na mradi ukwama
kufanya kazi kwa miaka hiyo yote na wahusika wako na wengine wako wizara ya
mifugo na kilimo hilo halitavumiliwa kamwe lazima hatua zichukuliwe haraka.
Alisema
TAKUKURU inapaswa kuchukua hatua kwa kuwasaka wale wote waliohusika kukwamisha
mradi huu kwa kutafuna fedha hizo na kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya
dola kujibu mashitaka.
‘’Haiwezekani
watu wanakula fedha za wafadhili ambao wana nina nzuri na nchi halafu
tunawaacha hilo sio kwa serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na
Rais Dkt John Magufuli’’
‘’Lazima
wale wote waliokula fedha za wafadhili wanapaswa kukamatwa mara moja na hiyo
nawaachia TAKUKURU ndani ya siku chache zijazo nahitaji majibu kuwa wamekamatwa
na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yao’’ alisema Gambo
Meneja
wa AWF, Fidelis Ole Kashe alisema lengo la kujengwa kwa machinjio katika shamba
hilo ni pamoja na kupanuaa wigo wa vyazo vya mapato yanayotokana na kuuza mifugo
na nyama iliyo bora katika kiwanda hicho na kutoza ushuru wa pango kutoka kwa
mwekezaji atayefanikiwa kuendesha machinjio hayo.
Sambamba
na hilo Kashe alisema kuwa kiwanda hicho cha machinjio kitatoa soko la kuuza
mifugo na nyama katika vijiji vinavyozunguka machinjio na pia ajira itatolewa
kw wananchi ikiweka kipaumbele kwa jamii zilizo jirani na machinjio hayo.
Kashe
alisema kuwa mapungufu yaliyopo katika mradi huo ni pamoja na kutolewa fedha
nyingi lakini hadi sasa mradi huo kushindwa kukamilika, kukosekana kwa
mwekezaji,vifaa vilivyotumika kujenga havina ubora, mradi haukuwekewa mipango
endelevu na wafadhili kusitisha kutoa fedha tena kumalizia mradi huo wakati
fedha zilizotolewa hazina maelezo zilitumikaje.
Mwisho