Katika mazungumzo yao walijadiliana ushirikiano kati Serikali ya Tanzania na falme za kiarabu ambapo programs maalumu ya Madaktari kutoka falme za kiarabu kwa kushirikiana na madaktari wa hapa nchini wataendesha hospitali zinazotembea (mobile hospitals) katika mikoa yote kwa kutoa huduma za Afya kwa Siku tano kila Mkoa kila mwezi.
Huduma hizi zitajikita zaidi katika Maeneo yasiyo na madaktari bingwa hususan magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari,magonjwa ya Moyo.
Mpango huu pia utahusisha Madaktari wanne toka Tanzania kwenda falme za kiarabu kwa mafunzo zaidi. Balozi alifuatana na madaktari,Dkt Adil Pishar na Dkt Atifa Girrlaini. Mpango huu ni wa mwaka mmoja,utaanza mwaka ujao 2017