Nyuma ya Balozi Seif Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum.
Makamu wa Rais wa Benki ya Kimataifa ya Exim ya Nchini China Bwana Sun Ping akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Nd. Khamis Mussa.
Kati kati yao ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Khalid Salu Mohamed.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Nd. Asha Ali Abdulla akisalimiana na Bwana Sun Ping kabla ya kuanza Mkutano wao.
Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akizunguma na Makamu wa Rais wa Benki ya Kimataifa ya Exim ya Nchini China Bwana Sun Ping Makao Makuu ya Benki hiyo Mjini Beijing Nchini China.
Bwana Sun Ping kulia akibadilishana mawazo na Mgeni wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara bnaada ya kumaliza mkutano wao Mjini Beijing China.
Picha na – OPMR – ZNZ.
Press Release:-
Benki ya Kimataifa ya Exim ya Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kusaidia Maendeleo ya Wananchi wake kupitia miradi tofauti inayoanzishwa.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo Bwana Sun Ping wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anayeuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa Serikali akimalizia ziara yake ya Kiserikali ya Siku Tano Nchini China.
Bwana Sun Ping alisema Taasisi hiyo ya Fedha ya China imeridhika na hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa na Zanzibar katika kuimarisha uchumi wake kiasi kwamba Benki hiyo itaangalia namna za kusaidia nguvu katika kuona miradi inayoanzishwa inatekelezwa.
Makamu wa Rais wa Benki hiyo ya Exim alimueleza Balozi Seif na Ujumbe wake kwamba Tanzania ndio nchi pekee iliyopewa kipaumbele na benki hiyo katika kupatiwa mikopo na misaada ikilinganishwa na Nchi nyengine Barani Afrika.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Benki hiyo ya Exim kwa ukarimu wake wa kuunga mkono miradi ya Maendeleo inatotekelezwa na Zanzibar kwa njia ya misaada na hata mikopo.
Balozi Seif alisema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana miongoni mwa Wanachi waliowengi Zanzibar kufuatia kuibuka kwa miradi kadhaa ya Kiuchumi na maendeleo iliyopata msukumo kupitia Benki hiyo ya Kimataifa ya Exim.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
23/11/2016.