Home » » Magufuli aombwa kusaidia amani Sudan Kusini

Magufuli aombwa kusaidia amani Sudan Kusini

Written By CCMdijitali on Thursday, December 8, 2016 | December 08, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam Desemba 8,2016.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan Kusini, Rebecca Nyandeng Garang de Mabior, Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

Baada ya mazungumzo hayo, mke huyo wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan Kusini, Rebecca Mabior alisema yeye na ujumbe wake wamelazimika kufika nchini Tanzania kuonana na Dk Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa EAC kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan Kusini, huku wakimuomba ashirikiane na viongozi wenzake wa EAC kuisaidia Sudan Kusini kutafuta suluhisho la mgogoro unaolikabili taifa hilo.

“Tumefarijika kuwa hapa katika Ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi Rais Dk Magufuli kama Mwenyekiti wa jumuia ya Afrika ya Mashariki akishirikiana na viongozi wenzake wa jumuia hiyo kuona namna gani wanaweza kutusaidia ili Taifa la Sudan Kusini liwe Taifa lenye amani.

“Hivyo hapa tunawakilisha vilio vya watu wa nchi yetu na kikubwa tunachokitaka ni Amani katika nchi yetu na hiki ndio kilio chetu,” alisema Mama Rebbeca Mabior.

Naye Rais Magufuli amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan Kusini kutafuta njia mwafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani na ili kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa Taifa hilo.

“Mama Rebecca hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea katika nchi ya Sudan Kusini hivyo, ningezisihi pande zote zinazotofautiana kumaliza tofauti zao kwa amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa la Sudan Kusini,” alieleza Rais Magufuli kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu.

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mabior Garang Mtoto wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Hayati John Garang De Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link