Home » » CCM yavuna wanachama wa CHADEMA 380 Tunduma kwenye maadhimsiho ya Miaka 40

CCM yavuna wanachama wa CHADEMA 380 Tunduma kwenye maadhimsiho ya Miaka 40

Written By CCMdijitali on Sunday, February 5, 2017 | February 05, 2017


WANACHAMA 380 katika Mji wa Tunduma Mkoani Songwe, kutoka vyama mbalimbali vya upinzani kikiwemo chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, wamejiunga na chama cha Mapinduzi

CCM wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 40 tangu kuzaliwa kwa chama hicho, wakidai kufurahishwa na utendaji kazi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk John Pombe Magufuli.

Sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi katika Mikoa ya Mbeya na Songwe zimefanyika katika Mji wa Tunduma Mkoani Songwe jimbo ambalo ni ngome ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo Chadema ,ambapo Chama cha mapinduzi kimefanikiwa kuvuna wanachama 380,ambao wamerejesha kadi za vyama vyao na kupewa kadi za CCM lakini wakaomba ulinzi zaidi.

Mwenyekiti wa CCM katika Mikoa ya Mbeya na Songwe ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akaagiza wakuu wa mikoa ya Mbeya na Songwe kuwachukulia hatua za kisheria wanaotishia usalama wa wengine.

Awali maadhimisho haya yameaanz na upandaji wa miti katika shule ya msingi Manga iliyopo Mji mdogo wa Tunduma.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link