Home » » Kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo na Wadau wa Habari .

Kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo na Wadau wa Habari .

Written By CCMdijitali on Friday, February 3, 2017 | February 03, 2017

 Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mashaka Mrisho Gambo amefungua Kongamana kutoa taarifa ya maendeleo katika Mkoa wa Arusha ambapo kongamano hilo limewashirikisha wadau wa habari katika kuangalia na kutafakari na kupitia pamoja na kuangalia mpango mkakati wa maendeleo katika Mkoa.

Gambo amesema kuwa kongamano hilo lina lengo la kutoa mrejesho kwa Watanzania kupitia waandishi kwa kipindi cha miezi sita ,na kuangalia mambo gani serikali ikiyapa kipaumbele itaondoa changamoto mbalimbali katika jamii kwa ujumla.

Aidha amesema kuwa utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miezi sita hadi kufikia desemba 2016 umekuwa na mafanikio makubwa ,ambapo amesema kuwa hii ni kutokana na utamaduni wa kufanya na kutekeleza majukumu ya kazi kwa vitendo.

Amesema utekelezaji huo umechangia katika kuboreka kwa maeneo mbalimbali ya sekta muhimu katika kukuza uchumi katika mkoa hasa pato la mkoa na wananchi moja kwa moja.

“Katika kipindi hiki,miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa na kupewa kipaumbele cha kutosha hivyo kwa namna moja kutekeleza mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini (MKUKUTA II)katika mkoa na taifa kwa ujumla”alisema Gambo.

Amesema kuwa Mkoa umesimamia utekelezwaji wa shughuli za serikali na kushuhudia mafanikio katika sekta za kilimo,afya,maji,barabara,mofugo,maliasili na nyinginezo kama takwimu zilivyowasilishwa .

Amesema kuwa serikali imejipanga kuhangaika na wale wote ambao wanachochea migogoro kwa wananchi na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi hatutawafumbia macho.

Kwa upande wamafanikio utekelezaji wa mkoa kuanzia mwaka 2005 mkoa ulikuwa na shilingi 723,809 milioni kwa mwaka huo mkoa ulikuwa wa (9) katika kuchangia patao la Taifa,ambapo pato la mkazi lilikadiriwa kuwa shilingi 506,902 kwa mwaka sawa na shilingi 1,389 kwa siku.

Kwa mwaka 2010 pato la Mkoa wa Arusha lilikuwa shilingi 2,136,514 milioni kwa kuchangia pato la taifa Arusha ilikuwa ya 7.mwaka huo pato la mkazi wa Arusha lilikuwa shilingi 1,283,361 kwa mwaka sawa na shilingi 3,516 kwa siku.

Hadi mwaka 2015 pato la mkoa linakadiriwa kuwa shilingi 4,271,447milioni.

kwa takwimu hizo pato la mkazi wa Arusha lilikuwashilingi 2,322,031 milioni kwa mwaka ni sawa na shilingi 6,361 kwa siku.

Mkurugenzi wa Kituo cha mikutano cha kimataifa AICC Elishilia Kaaya akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo na yeye kama mwenyeji wa eneo hilo akiwakaribisha katika kituo hicho.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano ambalo aliwaahidi waandishi kuwa ataliiitisha kwa ajili ya kujadili na kupata taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha pamoja na wadaumbalimbali.

Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizungumza katika kongamano hilo .

Mwenyekiti wa Arusha Press Club (APC) Akizungumza na katika kongamano hilo.

Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa maendeleo katika komgamano hilo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia akieleza baadhi ya mambo ambayo Halamashauri ya Jiji imeyafanya katika Kongomano hilo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.

Wadau wa Utalii kutoka TANAPA wakiwa katika kongamano la wadau wa habari mkoa wa Arusha .

Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Arusha Ndg Shaaban Mdoe akiwa na baadhi ya wadau wa habari Mkoa wa Arusha.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.

Wakuu wa Idara na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ,akiwa kwenye kongamano katika kituo uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano AICC katika ukumbi wa Mbayuwayu.

Wadau wa Utalii kutoka TANAPA wakiwa katika kongamano la wadau wa habari mkoa wa Arusha .

Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua,Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Ndg Athmani Kihamia na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ,akiwa kwenye kongamano katika kituo uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC katika ukumbi wa Mbayuwayu.

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano hilo na Waandishi wa Habari.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akiteta jambo na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabrielly Daqarro, kwenye kongamano lilofanyika katika kituo uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC katika ukumbi wa Mbayuwayu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akiteta jambo na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua, kwenye kongamano lilofanyika  katika kituo uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC katika ukumbi wa Mbayuwayu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Ndg Athmani Kihamia (katikati) na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua wakiteta jambo nje ya Ukumbi wa Mkutano kaika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha AICC.

Picha na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha ,Ndg Jasper Kishumbua 0784-463332

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link