MADIWANI WAJIFUNGIA MASAA 5 KUHUSU KUMKATAA MKURUGENZI WA JIJI BW. ATHUMANI KIHAMIA.
Madiwani hao wakiongozwa na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema walijiorodhesha majina kwa idadi ya theluthi moja ya madiwani wote kwa lengo la kuitisha baraza maalum la kumkataa mkurugenzi huyo ambaye wanamtuhumu kuwa tangu alipoingia amekuwa na Kazi moja ya kuvuruga madiwani wa Chadema.
Awali desemba 2016 TAMISEMI iliunda tume ya watu 5 kufuatilia utendaji kazi wa mkurugenzi huyu lakini bado habadiliki. Madiwani hao hivi karibuni mnamo tarehe 23 juni 2017 walijifungia katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri kumjadili mkurugenzi huyo kwa tuhuma za kupuuza maazimio ya vikao na kutekeleza ya kwake na washirika wake. amekuwa akiwaweka ndani ndani madiwani kwa kutumia polisi na kulazimisha maamuzi yasiyo ya madiwani kuhusu upangishaji wa maduka ya jiji na kutowaondoa wamachinga mjini na mengineyo mengi. Baada ya mjadala mzito yafuatayo yaliamuliwa dhidi ya mkurugenzi huyo.
- Apelekwe kwenye kamati ya maadili inayoongozwa na Profesa Mosha ili asomewe tuhuma hizo za kuendesha halmashauri kibabe.
2. Baada ya hapo baraza maalum la madiwani kuitishwa na kumsomea tuhuma na kumkataa siku hiyohiyo.
3. Endapo maamuzi ya kumkataa yakipuuzwa baraza la madiwani litavunjwa kuliko kuendelea kuongozwa na mkurugenzi huyu ambaye hatabiriki na haeleweki anachokitaka.
4. Kama ilivyo kwa RC Mrisho Gambo mkurugenzi huyu amekuwa akiundiwa tume na hata kupelekwa PCCB kila Mara hasa alipokuwa Kaliua mkoani Tabora kwa kuvurugana na madiwani na kukataa kutekeleza maazimio ya vikao ambapo alipohamishwa walifanya sherehe.
5. Baraza likivunjwa itatengenezwa migogoro Ili mabaraza mengine ya halmashauri zinazoongozwa na Chadema zivunjwe kisha maandamano yaanze nchi mzima.
Akiongea na chanzo hiki diwani mmoja wa viti maalum Chadema amesema kwa ufupi mitego yote ya kumnasa Mkurugenzi huyu ni kama imeshindikana ikiwemo kumtegeshea asaini nyaraka zenye utata kwa kuwatumia wakuu wa idara au kumtengenezea ajali ya gari au kumteka au kumchafua ikiwemo kumteka mwalimu Batuli Kisaya wa shule ya msingi ya Unga limited.
"Tukifika 2020 na huyu mtu tutaharibikiwa ni vyema mgogoro iwe mikubwa ili mheshimiwa rais amtoe vinginevyo bora kuvunja baraza kuliko kuingia katika uchaguzi akiwepo maana hatutabaki salama damu itamwagika kwa kuwa anafahamika akipewa maagizo na serikali anatekeleza kama yalivyo hapunguzi hata nukta ni hatari hakutakuwa na haki hata kidogo" alisema mbunge Lema.
Rafiki wa karibu wa mmoja wa wasaidizi wa karibu Mkurugenzi Huyo amethibitisha kuwa kwa jinsi alivyo tangu amefika hajabadilika wala kuonyesha dalili za kubadilisha misimamo yake, kwa kweli kazi ipo.