WANACHAMA 26 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kuwania uenyekiti wa chama hicho mkoani Shinyanga akiwamo aliyewahi kushikilia wadhifa huo na mkuu wa wilaya wa zamani, Charles Gishuli, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige pamoja na wanawake wawili.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Haula Kachwamba alisema jana kwamba wagombea wote waliochukua fomu wamerudisha kwa wakati. Alieleza kuwa katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wapo wanachama 12, wajumbe wa NEC Taifa Tanzania Bara wapo 12 na sita wanataka kuwa Katibu wa Siasa na Uenezi.
Kachwamba alisema wanawake wawili ambao ni Angela Joseph na Juliana Billu wamejitokeza kuwania nafasi ya Uenyekiti pamoja na Gishuli na wagombea wengine ambao ni Michael Bundala, Khalfani Mandwa, Sendema Luhende, Nassoro Waryoba, Charles Simon, Bathromeo Mwanansia, Joseph Raulent na Justine Sheka.
Pia wamo Maxmine Mazulla, Erasto Theonest, Shija Malisha, Luhende Richard, Emmanuel Mlimandago, Mabala Mlolwa, Jonh Makune, Salumu Simba, Swetbert Nkuba, Cornel Ngudungi, Ally Manzi, Festo Kang’ombe, Nuhu Mnoni, Ezekiel Maige na Thomas Chuma.
Aliwataja wanaotaka NEC Taifa ni Richard Luhende, Sweetbert Nkuba, Mola Zabroni, Mussa Jonas, Abed Aljabri, Gerad Mwanzia, Peter Daniel, Gasper Kileo, Margaye Makune, Bernard Shigella, Joyce Masunga na Solomoni Matoba.
Kwa upande wa NEC Tanzania Bara, waliojiotokeza ni James Masunga, Gikula Madulu, Donald Tilusasila, Hassan Mwendapole, Khalfan Mashimba, Awadhi Aboud, Abeid Aljabri, Emmanuel Luhende, Erasto Lushekya, Mussa Ngangalla, Saleh Sizya na Meshack Mashigalla. Aliwataja waliojitokeza nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi ni Msanii Masele, Margaye Makune, Maxmine Mazulla, Emmanuel Mlimandago, Jacqueline Brayi na Mussa Ngangalla.