Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Pikipiki
za Traffic 10, Computer 100 na Baiskel za kisasa 200 kwaajili ya
kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Polis Dar es Salaam na kulifanya
kuwa la kisasa.
Kupatikana kwa Vitendeakazi hivyo ni matokeo ya jitiada binafsi za RC Makonda kutafuta Wahisani.
Makonda amesema amedhamiria kuleta Mapinduzi Makubwa kwa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na Vifaa vya kutosha ikiwemo Magari, Pikipiki za kawaida na zile za Traffic,Baiskeli za Doria,Silaha na Computer ilikuwafanya kufanya kazi katika Mazingira mazuri.
Amesema amechoka kuona Askari wakipoteza Maisha wakitekeleza majukumu yao kwa kuvamiwa na Majambazi na kuporwa Silaha ndio maana anapambana kutafuta vitendeakazi ili Askari wake wajivunie kufanya kazi katika Mkoa wake.
Aidha amesema Pikipiki za Traffic zitaenda kusaidia kwenye Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha wagonjwa Hospital.
Kuhusu Computer 100 alizotoa amesema zitagawanywa kwenye Vituo vya Polisi 20 na kufungwa mfumo wa kisasa wa kupokea taarifa za Uhalifu, kubainisha maeneo yaliyoshamiri Uhalifu, kutambua wahalifu Sugu ambapo mfumo huo utatoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa,Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo ili kuwezesha Viongozi kufanya maamuzi.
Amesema Baiskeli 200 alizozitoa zitaendelea kuimarisha Doria mitaani na kuongeza kuwa Baiskeli nyingine za kisasa 1,000 zipo Nchini China zikifanyiwa Maboresho ambapo zikikamilika zitakuja kuongeza nguvu kupambana na Uhalifu.
Sanjari na hayo amesema Magari Mabovu 15 ya Polisi kati ya 26 yaliyopelekwa Kilimanjaro kufanyiwa marekebisho yamekamilika ambapo yatakuwa na Mwonekano wa kisasa kama ilivyo kwa Magari ya Jeshi ya UN.
Pamoja na kuligusa Jeshi la Polisi kama Taasisi ameona pia aguse maisha ya Askari mmoja mmoja kwa kuwatafutia Mkopo wa Viwanja sababu gharama ya Viwanja ni kubwa hivyo kufanya Askari kushindwa kumudu gharama hali inayosababisha baadhi yao kustaafu wakiwa hawana makazi na kuishi kwa tabu.
Viwanja hivyo vilikuwa vikiunzwa kwa Tsh 20,000/= kwa Square meter lakini RC Makonda amepambana hadi kufikia Tsh 5,000/= kwa Square Meter ambapo Askari watakuwa wakilipa mkopo huo kidogokidogo kwa muda wa Miaka Mitano na wataruhusiwa kujenga hata kama hawajamaliza mkopo wao.