Home » » WAZIRI MKUU AKUTANA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA NAMERA GROUP INDUSTRIES

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA NAMERA GROUP INDUSTRIES

Written By CCMdijitali on Tuesday, September 12, 2017 | September 12, 2017

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao. Waziri Mkuu amekutana naye leo Septemba 12/ 2017 Ofisini kwake Dar es Salaam.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.(L) Ni Meneja wa Namera Bwana Muhammad Waseem. Waziri Mkuu amekutana nao leo Septemba 12/ 2017 Ofisini kwake Dar es salaam. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
 

“Aahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini”
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.
Amekutana na Bw. Pardesi leo (Jumanne, Septemba 12, 2017) kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam na amesema kwamba tayari Serikali imeanza kuwahamasiha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.
Waziri Mkuu amempongeza Bw. Pardesi kwa kuiunga mkono Serikali katika mpango wake wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda. Kampuni ya Namera Group of Industries inamiliki kiwanda cha nguo cha NIDA na cha Namera vya jijini Dar es Salaam.Kampuni inatarajia kufungua kiwanda kingine cha nguo wilayani Kahama.
Pia Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha zao la pamba linapewa kipaumbe alikutana na wakuu wa mikoa yote inayolima pamba Ijumaa, Septemba 8, 2017 na aliwaagiza wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi hususan wakulima wa zao la pamba.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link