Home » » WAZIRI JAFO AVITAKA VITUO VYOTE VYA AFYA KUTENGENEZA BUSTANI ZA KUPUMZIKIA

WAZIRI JAFO AVITAKA VITUO VYOTE VYA AFYA KUTENGENEZA BUSTANI ZA KUPUMZIKIA

Written By CCMdijitali on Friday, December 29, 2017 | December 29, 2017

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo katika Manispaa ya Dodoma.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(Kushoto) akimsikiliza Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole kuhusiana na maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya.

 Jengo la Wodi ya Kinamama kama linavyoonekana likiwa linefikia katika hatua ya Lenta.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi(katikati) baada ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya Afya Katika Kituo cha Afya Makole.

Jengo la Chumba cha Upasuaji kama linavyoonekana likiwa katika hatua ya Lenta.
 
Nteghenjwa Hosseah, TAMISEMI.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amevitaka vituo vyote vya Afya Nchini sambamba na hospital za Wilaya kutengeneza bustani ya kupumzikia kwa wagonjwa wanaosubiria matibabu katika maeneo hayo.

Waziri jafo ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka uongozi wa Kituo hicho kutenegenza bustani ya kisasa pamoja na kupanda miti ya kutosha ili kutunza matunzingira lakini kupendezesha eneo la hospital.


“Hili Agizo liende kwa Vituo vyote Nchini pamoja na Hospital za Wilaya zilizoko chini ya TAMISEMI kuhakikisha wanaekeleza maelekezo haya katika ameneo yote nataka hospital iwe sehemu ya kupa faraja mgonjwa kwa kupata huduma nzuri lakini pia kusubiria huduma hiyo katika maeneo yanayovutia wakati wote” Alisema Waziri Jafo.

Akikagua majengo matano yanayojengwa katika Kituo hicho cha Afya na kusimamiwa na TAMISEMI Waziri Jafo amesema ameridhishwa na Ujenzi wa miundombinu hiyo ya Afya katika Hospital ya Makole kwani umefuata ramani zilizotolewa na Wizara, unajengwa kwa ubora na uko ndani ya muda wa Utekelezaji. 


“Hivi ndio ninavyotaka wataalamu wangu kujiongeza katika baadhi ya maeneo mfano hapa Mmejenga Mabara kubwa kulingana na wingi wa wagonjwa mnaowahudumia kwa siku sasa sio kwa sababu ramani imeonyesha maabara ndogo basi kila mtu anafuata hivyo hivyo ni lazima tujiongeze kulingana na mahitaji ya ameneo yetu ya huduma” Alisema Waziri Jafo.


Akizungumzia maendeleo ya mradi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole amesema Ujenzi huu umesema ujenzi wa Maabara, chumba cha Upasuaji, Wodi ya Kina Mama, Nyumba ya Mganga pamoja na Ukarabati wa Kichomea Taka utakamilika mapema mwezi February 2017 na Fedha zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi huo zitatosha na kukamilisha ujenzi wa miundombinu yote.


Kituo cha Afya Makole ni miongoni mwa vituo 211 Nchini vilivyopokea/vitakavyopokea Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya lengo ikiwa ni kuboresha Miundombinu ya Afya ili kuweza kutoa huduma bora kwa watanzania. 


TAMISEMI YA WANANCHI.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link