Home » » UVCCM Taifa wafanya dua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Aman Karume .

UVCCM Taifa wafanya dua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Aman Karume .

Written By CCMdijitali on Friday, December 29, 2017 | December 29, 2017

 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheir James(kushoto wa kwanza) akitoa Shukrani kwa mapokezi aliyopewa na Uongozi wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar chini ya usimamizi wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saasalla (Mabodi) pamoja na SMZ kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed kama wanavyoonekana katika picha hiyo.

 VIONGOZI mbali mbali wa UVCCM pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi wakiomba dua katika Kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume lililopo katika eneo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita (kusho) Msimamizi na mwandaji wa Vipindi vya Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Radio Suzan Kunambi (kulia) akimfanyia mahojiano kiongozi huyo kuputia kipindi cha Asubuhi na ZBC huko katika Studio za Shirika hilo Rahaleo Unguja.

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla(Mabodi) amewahakikishia Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM) kuwa ataendelea kushirikiana nao katika masuala mbali mbali ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Ahadi hiyo ameitoa wakati akizungumza na viongozi wa UVCCM Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti Kheir James na Makamu Mwenyekiti Tabia Maulid Mwita, waliofika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kwa ajili ya kutembelea na kuomba dua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume .


Dk. Mabodi aliwambia viongozi hao kwamba kumbukumbu na historia ya Marehemu Mzee Abeid karume inatakiwa kulindwa na vijana wa CCM ambao wao ndio viongozi wa sasa na baadae wenye dhamana ya kulinda serikali na Chama visichukuliwe na wapinzani.


Naibu Katibu Mkuu huo amemtaja Marehemu Mzee Abeid Karume kuwa alikuwa ni kiongozi wa Mapinduzi mwenyekiti aliyekuwa na azna kubwa ya busara na falsafa pana ya masuala ya uongozi na ubunifu ndani na nje ya ASP na Serikali kwa ujumla.


 Amesema Afisi Kuu ya CCM Zanzibar inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Dk.Ali Mohamed Shein itatoa ushirikiano kwa UVCCM pamoja na jumuiya na taasisi zote za kisiasa na kiserikali ili wananchi waendelee kupata huduma bora za kijamii, kichumi na kisiasa.


 Pia, ameueleza msafara huo wa viongozi wa UVCCM waliofika Zanzibar kwa mara ya kwanza toka wachaguliwe kupitia Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja huo Taifa, kwamba maendeleo yaliyopatikana visiwani Zanzibar yanatokana na juhudi za CCM kuisimamia Serikali itekeleze Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020.


“Kwanza karibuni sana Kisiwandui ambapo ndio sehemu pekee yenye historia na Ofisi za waasisi wetu wa Afro Shiraz Party (ASP), walioanzisha harakati za ukombozi wa Waafrika wa visiwa vya Zanzibar na hatimaye Januari 12, 1964 wakaung’oa utawala wa kisultani na kusimamisha Dola huru iliyojali maisha na utu wa watu wote.


Nyinyi vijana ni azna kubwa kwa chama chetu hivyo fanyeni kazi kwa ufanisi ili kulinda heshima na dhamana mnazopewa kwa lengo la kuwanufaisha vijana wenzenu ambao kwa njia moja ama nyingine hawajajaliwa kama zenu”, alisema Dk.Mabodi.


Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa , Kheir James amekipongeza Chama cha Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi zake za kuimarisha taasisi hiyo ya kisiasa licha ya kuwepo na changamoto za kisiasa zinazosababishwa na wapinzani.


Mwenyekiti Kheir amesema yupo tayari kufanya kazi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla ili changamoto mbali mbali zinazowakabili vijana ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu na taasisi hizo.

 MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Tabia Maulid Mwita ameishauri serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuongeza kasi katika usimamizi wa mamlaka zinazohusika na uendeshaji wa kesi za udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kuhakikisha zinatenda haki.


Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza katika kipindi Maalum kinachorushwa mubashara kila siku asubuhi na ridhaa ya Taifa ya Zanzibar ambayo ni Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC Radio) katika jengo la Shirika hilo lililopo Rahaleo Mjini Unguja.


Amesema miongoni mwa mikakati ya UVCCM ni kukemea vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, dawa za kulevya pamoja na vitendo viovu vinavyosababisha mmomonyoko wa maadili kwa vijana.
Tabia ameeleza kuwa Umoja huo umejipanga kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya taasisi hiyo kisiasa na kiuchumi.


Amesema wakati wa vijana kutumiwa kama ngazi ya kufikia mafanikio kwa baadhi ya watu umekwisha na badala yake vijana hao watumie fursa zilizowazunguka kujitafutia kipato.


“ Vijana tunatumiwa na baadhi ya wanasiasa hasa inapokaribia kipindi cha kampeni za uchaguzi na wanapopata nafasi hawaanzishi miradi ya maendeleo ya kulisaidia kundi hilo ambalo wengi wao hawana ajira za uhakika.


Sasa ifikie wakati na sisi tuwe na misimamo kwa kujiajiri wenyewe kupitia sekta ya ujasiria mali na ufundi na watushauri mambo mbali mbali ya kuimarisha taasisi yetu kisiasa.


Kupitia kipindi hicho Makamu Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa vijana wote nchini kuwaunga mkono viongozi wa Chama na Serikali hasa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwani viongozi wanaojali maslahi ya vijana.


Amesisitiza wananchi kuheshimu utawala wa kisheria kwa kuepuka uvunjaji wa sheria na miongozo mbali mbali ya nchi.


Pamoja na hayo amewataka viongozi wa UVCCM kuwa mfano wa kuigwa kivitendo, kauli, maadili, hekima na busara ili vijana wengine waliopo katika vyama vya upinzani wavutike na kujiunga na umoja huo.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link