Home » » HANDENI YAFANYA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI.

HANDENI YAFANYA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI.

Written By CCMdijitali on Wednesday, January 19, 2022 | January 19, 2022

 

Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen akiongea kwenye Baraza la wafanya kazi.









Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imefanya kikao cha baraza  la wafanyakazi Ili kupitia mpango wa rasimu ya bajeti  ya Halmashauri ya mwaka wa fedha 2022/2023.

Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen (Aliyevaa tai nyekundu) amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwatetea wananchi  hivyo watanzania na wafanyakazi  wote kwaujumla wazidi kumuombea Rais Afya njema Ili wazidi  kuuona upendo wake kwa wafanyakazi.

Bw. Saitoti amesema kuwa baraza  hilo ni muhimu kupitia rasimu hiyo ya bajeti ili kuboresha kabla ya kwenda  kujadiliwa kwenye baraza la madiwani pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza Walimu kwa kusimamia Miradi ya Ujenzi wa miundombinu ya Madarasa ya UVIKO-19 na Miradi yote inayotekelezwa kwenye shule zao.

Kwakumalizia Bw. Saitoti amewaasa watumishi kusimamia uadilifu na uaminifu kwenye mazingira yao ya Kazi.

Kwaupande wa viongozi wa vyama vya Wafanyakazi wameishauri Serikali kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya Kazi vizuri na wameomba kuboreshewa maslahi pamoja na mazingira bora ya kufanyia Kazi.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link