Tarehe Januari 17 2022 Waziri wa Fedha Mheshimiwa Mwigulu ametoa maagizo ya kikazi kwa Wakaguzi wa Ndani kote nchini kukagua fedha za miradi yote ya maendeleo zilizotolewa na Serikali katika maeneo yao na kuwasilisha taarifa ndani ya mwezi mmoja wakati akiwa kwenye Mkutano na Wananchi Kigoma,
"Nimeelekeza wakague fedha zote zilizotolewa wakiainisha miradi iliyotekelezwa, kiwango cha utekelezaji wa miradi, hatua iliyofikiwa katika utekelezaji na thamani ya miradi."
Serikali
ya Awamu ya Sita ndani ya muda mfupi imepeleka fedha nyingi kwenye
miradi ya maendeleo, hivyo matarajio ya Watanzania ni kuona matokeo
chanya ya fedha hizo kabla fedha zaidi hazijatolewa.
Kuanzia sasa Serikali haitainyima Halmashauri yoyote fedha kwa sababu ya Hati Chafu. Tutashughulika na wanaosababisha kupatikana kwa #HatiChafu ambazo zinakwamisha wananchi kupata maendeleo. - Waziri wa Fedha Mheshimiwa Mwigulu Nchemba