MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO ATEMBELEA NA KUKAGUA ZOEZI LA UPOKEAJI NA UANDIKISHWAJI WA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA NA AWALI KATIKA SHULE ZA MSINGI HALMASHAURI YA WILAYA YA LUSHOTO
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Ndugu Kalisti Lazaro
ametembelea na Kukagua Zoezi la Upokeaji na Uandikishwaji wa Wanafunzi
wa Darasa la Kwanza na Awali katika Shule za Msingi Halmashauri ya
Wilaya ya Lushoto.
Mkuu
wa Wilaya ametoa Maagizo kwa Waalimu Wakuu kuwa Wawapokee na
Kuwaandikisha Wanafunzi wa Darasa la Kwanza na Awali kama Utaratibu wa
Serikali unavyoelekeza na bila Kuwarudisha Nyumbani kwa Kutokuwa na Sare
za Shule na Kuwachangisha Wazazi Michango isiyo na Kibali.
Alieleza "Mwalimu wapokeeni Wanafunzi na Kuwaandikisha bila Masharti, Serikali imeweka Utaratibu Mzuri msiuvuruge, Kama Mwanafunzi hana Sare za Shule apokelewe na Mzazi wake apewe muda wa Kulitekeleza hilo bila Mwanafunzi kuzuiwa kuingia Darasani na Michango inayoruhusiwa ni ile tuu ambayo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeipitisha na kutoa Kibali cha Mchango"
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro akiwa Shule ya Msingi Mbula katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto |
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro akiwa Shule ya Msingi Mbula katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto |