KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Taifa, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amemtaja Rais Samia Suluhu
Hassan, kuwa turufu ya maendeleo ya Watanzania kutokana na falsafa
iliyobeba mambo matatu anayoyatumia katika uongozi wake.
Shaka
aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati akipokea tuzo ya
kumpongeza Rais Samia kwa utendaji mzuri, iliyotolewa na Umoja wa Vijana
wa CCM (UVCCM), Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alisema
Rais Samia amekuwa turufu ya maendeleo ya watanzania kutokana na
falsafa tatu anazozitumia katika uongozi wake ambazo ni upangaji,
utekelezaji na usimamiaji.
Kwa mujibu wa Shaka, hayo yamejidhihirisha katika uongozi wake kwa kipindi cha miezi tisa ambapo mambo makubwa yamefanyika.
Alieleza
katika kipindi hicho umeshuhudiwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025, kwamba wanaamini kufikia mwaka 2025
utekelezaji utazidi asilimia 100.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la UDSM, Isack Sambuli, alisema
uamuzi wao huo unatokana na kuguswa na mambo makubwa anayoyafanya Rais
Samia ambayo moja kwa moja yanawagusa wanafunzi wa elimu ya Juu na
Watanzania kwa ujumla.
Alisema miongoni mwa mambo hayo makubwa ni pamoja na kuongeza fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu.
Sambuli
alisema uamuzi wao huo haukulenga kutaka kutazamwa kwa ajili ya uteuzi
wa uongozi Bali wamelenga kutazama uhalisia wa mambo makubwa.
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi,
Shaka Hamdu Shaka, akipokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa
Vijana wa CCM,Tawi la UVCCM Seneti Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Ndg
Aizack Sambuli ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi
nzuri ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi,
Shaka Hamdu Shaka, akizungumza katika kongamano la kumpongeza Rais Samia
Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri ya kuleta maendeleo kwa
wananchi,iliyoandaliwa na Tawi la UVCCM seneti Chuo Kikuu Cha Dar Es
Salaam Ubungo, jijini Dar es Salaam leo tarehe 16 Januari,2022 katika
ukumbi wa Urafiki.
WANACHAMA wa UVCCM na CCM Tawi la UVCCM seneti Chuo Kikuu Cha Dar Es
Salaam Ubungo, jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Katibu wa Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka,
akipojea tuzo kwa ajili ya kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa
CCM, kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri ya
kuleta maendeleo kwa wananchi, jijini Dar es Salaam, (Picha zote na
Fahad Siraji wa CCM