Home » » WAZIRI UMMY AFANYA KIKAO CHA KAZI NA IDARA YA KINGA

WAZIRI UMMY AFANYA KIKAO CHA KAZI NA IDARA YA KINGA

Written By CCMdijitali on Monday, January 17, 2022 | January 17, 2022

Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu leo tarehe 17 Januari 2022 amefanya kikao cha kazi na Idara ya Kinga kwa kufanya mapitio ya pamoja kuhusu mafanikio, changamoto na vipaumbele vya Wizara katika kuimarisha huduma za Kinga nchini ili kuzuia maradhi na ulemavu na hivyo kupunguza gharama za matibabu na vifo miongoni mwa watanzania.
 
Waziri wa AfyaMheshimiwa Ummy Mwalimu amekutana na Watumishi wa Idara ya kinga na kujadili masuala mbalimbali ya kinga na malengo waliojiwekea ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Idara katika kuboresha utoaji huduma kwa wananchi wenye uhitaji.

Kikao hicho kimefanyika mapema leo Januari 17, 2022 katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe.

Katika kikao hicho, Mhe. Ummy amesisitiza juu ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi ili kupunguza kero na malalamiko katika jamii katika nyanja zote, ikiwemo katika huduma za mama na mtoto na huduma za lishe.  
 
 

Maeneo yalifayofanyiwa mapitio ni pamoja na; 

  1.  Epidemiolojia - Ufuatiliaji na Udhibiti wa magonjwa/matatizo yanayoathiri Afya ktk makundi ya watu 
  2.  Huduma za Chanjo kwa watoto (pamoja na Chanjo ya UVIKO) 
  3.  Afya ya Uzazi na Mtoto hususan kupunguza vifo vya wajawazito na watoto  
  4. Lishe bora 
  5.  Afya ya Mazingira ikiwemo ujenzi na matumizi ya vyoo bora 
  6. Elimu ya Afya kwa umma.
Pia wamejadili mikakati mbalimbali ya mapambano dhidi ya UVIKO19, Malaria,UKIMWI, TB na Magonjwa yasiyopewa kipaumbele (NTDs). 
Na kusisitiza kuweka msukumo zaidi katika huduma za Kinga
 












 

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link