📹Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu wakati
akiongea na watumishi wa Idara ya tiba ambapo amewataka kuchagua miradi
michache ya kutekeleza kwenye hospitali za rufaa za Mikoa ambayo inaweza
kumalizika kwa wakati na kukidhi haja za wananchi
Na. WA-Dodoma
Hospitali
za rufaa za mikoa nchini zimetakiwa kuboresha huduma za afya pamoja na
kuwa na mawazo mapana katika kuboreshaji wa miundombinu ya hospitali
hizo ili kuweza kuisaidia na kuipunguzia mzigo hospitali ya Taifa ya
Muhimbili,
Hayo yamesemwa
leo na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiongea na wafanyakazi
wa idara ya tiba ikiwa ni mwendelezo wa kukutana na kufanya mapitio ya
idara mbalimbali zilizopo kwenye wizara hiyo
Mhe.
Ummy amesema ili kuonesha kweli idara ya tiba ndio inayobeba wizara
hiyo hamna budi kuboresha huduma hizo ili zilingane na mahitaji ya
wananchi kwani wananchi wanaziamini hospitali za umma.
“tunatakiwa kuhakikisha utoaji wa huduma za afya ni mzuri, hivyo ni wakati wa kuangalia changamoto na kuziboresha ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao wanafika kwenye vituo vyetu kupata huduma“ amesema Mhe. Ummy.
Aidha, Waziri huyo
ameitaka idara hiyo kufanya upya mapitio ya miongozo ya utoaji huduma
ili kufanya huduma zinazotolewa kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa
zinakuwa bora na zenye manufaa kwa wananchi vilevile miongozo hiyo iweze
kuunganisha vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Hata
hivyo Waziri Ummy amewataka watumishi wa idara hiyo kufanya kazi kama
timu na endapo kuna changamoto ni vyema zikajadiliwa kwa pamoja ili
kwenda kwa pamoja katika kuboresha huduma za afya nchini.
#AfyaKwanza
#HudumaBoraKwaMtanzania