Home » » MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO AZINDUA MRADI WA MADUKA YA BIASHARA YA JESHI LA MAGEREZA WILAYA YA LUSHOTO

MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO AZINDUA MRADI WA MADUKA YA BIASHARA YA JESHI LA MAGEREZA WILAYA YA LUSHOTO

Written By CCMdijitali on Tuesday, January 18, 2022 | January 18, 2022

 

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro akizindua Mradi wa Maduka ya Biashara ya Jeshi la Magereza Wilayani Lushoto 18 Januari 2022

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro akisaini kitabu cha Wageni kwenye Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi kwenye Ofisi za CCM alipokuwa akielekea kwenye uzinduzi wa Mradi wa Maduka ya Biashara ya Jeshi la Magereza Wilayani Lushoto 18 Januari 2022

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro akitoa nasaha mara baada ya kuzindua Mradi wa Maduka ya Biashara ya Jeshi la Magereza Wilayani Lushoto 18 Januari 2022







Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro amezindua Mradi wa Maduka ya Biashara na Kutembelea na Kukagua Mradi wa Kufyatua Matofali na Mradi wa Ujenzi wa Nyumba na Ofisi za Maafisa Tarafa na Kutembelea eneo la Jeshi la Magereza Wilaya ya Lushoto lililotengwa kwa ajili ya Kujenga Gereza Jipya huko Yogoi.


Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Maduka ya Biashara Mkuu wa Gereza Wilaya ya Lushoto Kamanda SSP Hamis Ngaukia alisema " Kituo chetu kinaendelea na Miradi mbalimbali ya Kiuchumi na Maendeleo. Miradi hiyo ndiyo huwezesha shughuli za Kituo ikiwemo Miradi mingine Kuendesha Miradi mingine. Baadhi ya Miradi tuliyokuwa nayo ni pamoja na Mradi wa Vibanda vya Biashara ambao utaufungua leo hii, Mradi wa Ujenzi wa Nyumba na Ofisi za Maafisa Tarafa, Mradi wa Huduma kwa Jamii na Mradi wa Kufyatua Matofali (huu umekamilika kwa 80% na tunatarajia kuuanza wakati wowote kuanzia sasa). 

Ujenzi huu umetumia Mapato ya Vyanzo vyetu vya Ndani na Misaada kutoka kwa Wadau mbalimbali. Mradi huu umegharimu kiasi cha Tsh 40,000,000/=. Mbali na hayo tulipata Msaada wa Mbao na Mgodi wa Kupasua Mawe kutoka katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto.

 Vilivile tumetumia Tofali za Kuchoma ambazo tumefyatua na kuzichoma wenyewe" aliongezea " Ndugu Mkuu wa Wilaya, Fedha za Kutekeleza Mradi huu tumezipata kupitia Kazi za Ujenzi wa Nyumba za Maafisa Tarafa, Kusafisha Njia za Umeme na Huduma kwa Jamii (Vibarua). Vibanda utakavyovifungua leo hii ni Vibanda 12 na vyote tayari vinawapangaji ambao wamelipa Kodi ya Pango Tsh 80,000/= kwa Mwezi.


Mkuu wa Wilaya aliwapongeza Jeshi la Magereza Lushoto kwa kuwa na Uthubutu na Wabunifu na kutafsiri kwa Vitendo Kaulimbiu ya Jeshi la Magereza ambayo ni "FIKRA MPYA, MTAZAMO MPYA, KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KUJITEGEMEA". Pia alihaidi Kuendelea Kushirikiana na Jeshi la Magereza Wilaya ya Lushoto na endapo zitatokea Kazi za Serikali zinazo husu Ujenzi basi Jeshi la Magereza litapewa Kipaumbele. Pia alilitaka Jeshi la Magereza kuendelea kubuni Miradi mbalimbali ya Kiuchumi itakayowaingizia Kipato na Kuwawezesha Kujiendesha

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link