BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida limepitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2022/2023.
Na Ahmed M,Kiomboi
Mpango
huo umepitishwa katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika jana
katika ukumbi mdogo wa Halmashauri hiyo ambapo limepitisha Rasimu ya
Bajeti yenye makisio yenye thamani ya Sh.41,163,999,997.24 Bilioni
katika bajeti hiyo kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo
Michael Matomora alisema katika rasimu fedha kutoka mapato ya ndani
Sh.5,384,746,533.24, ruzuku ya Serikali ni 25,407,823,634.10 huku
wahisani ikiwa ni Sh10,371,426,830.
Alisema mwaka ujao wa fedha
wa 2022/ 2023 halmashauri hiyo imekisia kutumia jumla ya
41,,163,996,997.24 kutokana na vyanzombalimbali.
Alisema kutoka
mapato ya ndani wametenga Sh. 23,,526,000, matumizi ya kawaida
Sh.2,143,494,086.24, miradi ya maendeleo,3,217,726,444 jumla ya mapato
ya ndani ikiwa ni Sh.5,384,745,533.24.
Akielezea ruzuku ya
Serikali alisema mishahara ni Sh.20,418,014,391, matumizi ya kawaida Sh.
1,000,776,000,miradi ya maendeleo Sh.3,989,033,243 jumla ikiwa ni Sh.
25,407,823,634.
Alitaja fedha kutoka kwa wahisani ni Sh.10,371,426,830 huku jumla yake ikiwa ni Sh. 41,163,996,997.24.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba Innocent Msengi
aliwapongeza madiwani kwa kupitisha rasimu hiyo ambayo ameitaja kuwa ni
ya kipekee na ya mfano.
"Nitumie nafasi hii kuwapongeza madiwani
kwa kuandaa rasimu hii nzuri na ya kipekee hivyo nawaombeni mkaitekeleze
katika kukusanya mapato ili tuwenze kusonga mbele" alisema Msengi.
Mkuu
wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda alishukuru madiwani hao kwa
kupitisha rasimu hiyo na akatumie nafasi hiyo kuwaomba madiwani hao
kwenda kuhimiza wananchi wao kujitokeza kwa wingi wakati wa zoenzi ya
sensa ya watu na makazi na anuani za makazi.
Katibu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba, Ephrahimu Kolimba aliwaomba madiwani
hao kwenda kuzisimamia vizuri fedha hizo na akataka kuwepo na mashindano
ya kuwashindanisha kwa utendaji kazi wao na washindi wapatiwe zaidi
pamoja na wananchi wao waliofanya kazi husika.