Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti
Zelothe Stephen(aliyevaa miwani) |
KAMATI YA FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA HALMASHAURI.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati
ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh.
Mussa Mwanyumbu (Aliyevaa Shati rangi ya njano) ameongoza kamati hiyo
kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na
Halmashauri.
Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa jengo la Makao Makuu
ya Halmashauri, Ujenzi wa Maabara kwenye Shule ya Sekondari Mazingara,
Miundombinu ya uvunaji maji katika shule ya sekondari Mazingara, ujenzi
wa Shule ya Kata ya Mkata, Ujenzi wa Zahanati ya Pozo pamoja na ujenzi
wa jengo la zahanati ya Kwedikabu iliyopo kata ya Kwamsisi.
Wakati wa ziara hiyo kamati hiyo imempongeza Mkurugenzi wa Halmashuri na watumishi kwa kusimamia miradi hiyo kwa ukamilifu.
Aidha,
kamati hiyo ya Fedha, Uchumi na Mipango imeshauri Halmashauri kuwa
thamani ya fedha zinazotekeleza miradi hiyo lazima iendane na ubora wa
miradi hiyo na kuhimiza wanachi kujitokeza kufanyakazi kama nguvukazi ya
jamii kwani miradi hiyo inayotekelezwa ni ya wananchi.
Pia kamati
imeshauri kila mtaalam afanyekazi kulingana na utaalam wake ili
kufanikisha miradi hiyo kwa haraka na kwaufanisi mzuri.
Kwaupande wa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti
Zelothe Stephen ameishukuru kamati ya fedha, uchumi na mipango kwa
kufanya ziara ili kujionea miradi inayotekelezwa na Halmashauri na
amepokea ushahuri wote wa kamati na kuufanyia kazi.