UJENZI WA HOSPITALI YA MKOA SINGIDA ULIOKWAMA UANZE BAADA YA SIKU 7 -KATIBU MKUU AFYA .
Na.WAF-Singida
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameagiza mradi wa ujenzi wa jengo
la Magonjwa ya mlipuko la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
uliokwama uendelee mapema baada ya siku saba.
Ametoa
maagizo hayo leo Mkoani hapa mara baada ya kutembelea ujenzi katika
Hospital hiyo na kukutana na Katibu Tawala wa Mkoa, wajumbe wa Bodi ya
ushauri ya Hospitali, uongozi wa Hospitali, mshauri elekezi na
mkandarasi.
Mradi wa ujenzi wa jengo hilo ambao ulianza mwaka 2014, umeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali.
Katika
hatua nyingine Prof. Makubi ametoa muda wa siku saba kufungwa kwa mradi
unaoendelea wa ujenzi wa ghorofa chini ya Mkandarasi ambaye muda wake
pia umeisha na kukiagiza kitengo cha ununuzi na ugavi cha Wizara yake
kuhakikisha kuwa mkandarasi wa kuendelea na kazi ya ujenzi anapatikana
ndani ya siku saba hadi 14 ili kuendelea na
ujenzi wa awamu ya pili ya kujenga ghorofa ya kwanza wa jengo hilo.